Southern Tanzania Elephant Program
Dedicated to creating a secure future for elephants in southern Tanzania, and beyond
28/02/2026
๐๐ฃ๐ฎ๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐๐ญ๐๐ฅ๐ฅ๐ข๐ญ๐ ๐ค๐ฐ๐ ๐๐ฅ๐ข๐ง๐ณ๐ข ๐๐ฆ๐๐ซ๐ ๐ฐ๐ ๐๐ฌ๐ก๐จ๐ซ๐จ๐๐
Mnamo Januari 2026, timu ya VGS inayofanya kazi katika Shoroba ya Wanyamapori ya NyerereโUdzungwa ilikamilisha mafanikio ya ๐ฆ๐๐๐ฎ๐ง๐ณ๐จ ๐ฒ๐ ๐ฏ๐ข๐ญ๐๐ง๐๐จ ๐ฃ๐ฎ๐ฎ ๐ฒ๐ ๐ฆ๐๐ญ๐ฎ๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐ฒ๐ ๐ฏ๐ข๐๐๐ ๐ฏ๐ฒ๐ ๐๐๐ซ๐ฆ๐ข๐ง ๐ข๐ง๐๐๐๐๐ก.
Mafunzo haya, yaliyoandaliwa na Southern Tanzania Elephant Program (STEP) na kufundishwa na Meneja Msaidizi wetu wa Uhifadhi na mtaalamu wa GIS, ๐๐จ๐ฅ๐จ๐ฆ๐จ๐ง ๐๐๐ฆ๐๐จ๐ฌ๐ข, yaliwapa washiriki ujuzi muhimu wa mawasiliano ya wakati halisi, urambazaji kwa kutumia GPS, jinsi ya kutuma eneo ulilopo( location sharing), na matumizi ya mfumo wa tahadhari za dharura.
Vifaa vya Garmin inReach vinatumia muunganisho wa satelaiti, vinavyowawezesha wafanyakazi wa uwandani kutuma ujumbe, kufuatilia mienendo ya doria, na kutuma tahadhari za SOS hata katika maeneo ya mbali yasiyo na mtandao wa simu, hii inafanya kifaa hiki kuwa zana muhimu kwa ulinzi wa shoroba na ufuatiliaji wa wanyamapori.
Tathmini zilizofanywa kabla na baada ya mafunzo zilionyesha maboresho makubwa katika ujuzi wa kutumia vifaa hivi na kuongezeka kwa kujiamini katika operesheni za shoroba.
Shukrani nyingi kwa , Solomon kwa ufundishaji wa kina, na washiriki wote waliowezesha mafanikio ya mafunzo haya!
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Address
P. O. Box 2494
Iringa