Habari Za Soka
Tunajadili na kukupa updates za football kutoka pande zote za dunia.
18/12/2025
SIKU YA MAJONZI VALDEBEBAS MPAKA PLAZA DE CIBELES JIJINI MADRID
Wale wataalam wa Historia, wanadai falme iliyowahi kudumu kwa muda mrefu nchini Korea ni Joseon Dynasty kuanzia 1392-1897. Watu wa mziki wanaamini ngoma ya Ugali ya Juma Nature bado inaishi miongoni mwetu japo Nature sio yule tena, binafsi naamini 'Mtazamo' mkono wa Afande sele itabaki nasi japo Afande sio yule tena
Waswahili wa Pwani husema kila kitabu na zama zake, Wahehe kutoka Iringa wanasema 'Nothing is permanent' YES!
Ilikuwa Kuitazama Real Madrid sio issue sana ila utizamapo Madrid hakikisha umetupa macho kwa Nahodha Sergio Ramos kisha kwenye kiungo pale kwa Luka Modric kutoka nchi ya Kijamaa ya Croatia
Sergio Ramos kutoka Kusini mwa Hispania, Jijini Sevilla kwenye jimbo la Anderlucia, ni moja kati ya mabeki wachache sana kuwaona Ulimwenguni, Madrid watapata kisiki k**a kile?? Kwenye dunia hii yenye watoto mabishoo wengi, bado napata shaka
Luka Modric aliyesafiri kutoka mbali kutoka Mashariki mwa Ulaya mpaka Magharibi kote kueneza soka la burudani, tafsiri sahihi ya number 10, nae kashaaga na kuondoka yuko zake milan
Nizzo Forlove ananiambia Madrid wamepita watu bhana, Gento, Ferenc Puskas, Alfredo Di Stephano, Raul Gonzalez na Cristiano Ronaldo, lakini bado Ufalme uliweza kudumu, sipingani nae ila vipi kuhusu mabadiliko ya soka la kisasa, vipi kuhusu Sera ya Galacticos inawalipa kwasasa?? Jovic, Hazard, Diaz kwa pamoja wameifelisha kalamu ya Almasi ya Perez
Mabadiliko ya soka yanailazimu Madrid icheze k**ari kwa makinda, walienda Santos kumchukua Rodriygo, Vinicius wa Flamengo, Valverde kutoka Uruguay na sasa mbappe kutoka psg , Madrid wapo kwenye sera ya trial and error, Perez anawaza, Mariano Rajoy anawaza tutoke vipi?
Sipati picha hiyo siku miamba hii inarudi na kuaaga pale mazoezi Valdebebas, sipati picha sura ya alonso siku hiyo, wakati wanaenda kupiga makofi na kupata standing aviation pale Bernabeu, Madridista watalia mno
Mitaa ya Co**ha Espina itawakumbuka, Sanamu la Mwanamama pale Plaza de Cibeles litahuzunika, masela wa Calle de Alcala na Paseo Del Prado wote watahuzunika, Galacticos wanasepa zao, Sergio anarudi zake Sevilla na Luka anaenda kusabahi Croatia
02/12/2025
Ipo siku MO ataondoka zake Simba na kutuachia timu yetu japo sitegemei litokee ila naliona likitokea, ipo siku GSM ataachana na Yanga na kutuachia timu yetu japo sitegemei likitokea ila naliona likitimia
Ipo siku watu wenye maono na fedha zao watatuachia timu zetu k**a tu*iitavyo, lakini najua haujawahi kuwaza watatuachia somo gani kubwa, tumeshafunua chungu na kuchungulia yajae?? Tushawahi kutoka nje ya box na kuwaza zaidi?
Wananiachia somo kuwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na TP Mazembe ni miongoni mwa timu chache Kusini mwa jangwa la Sahara kubeba ubingwa wa Afrika, zote ni timu zinamilikiwa na Maboss, Patrick Motsepe na Moise Katumbi, nimejifunza kitu
Wapo wasiotaka kuchungulia mbali watasema mfumo wa Hisa sio rafiki, ila mwambie kuwa Hispania klabu zao zote 20 ni timu tatu tu za Wanachama, Real Madrid, Barcelona na Bilbao zingine zote 17 ni mfumo wa hisa, tunataka kuwa k**a Madrid na Barcelona?? Kato sidhani
Real Madrid ili uwe Rais na Mjumbe kuna kitu kinaitwa means testing, Mgombea una mali gani, utajiri gani hii ina maana kubwa kwao wanataka maono makubwa ya kiuchumi, bado kuna kundi la Wanachama wanaitwa Socios, wawakilishi wa Wanachama zaidi ya million moja kwenye maamu*i ya klabu
Najua kwa zengwe zetu hawa watapita na kwenda zao, na sisi tumebaki na fikra zetu za kijamaa kwenye dunia ya kibepari, sioni Simba wala Yanga wakipiga hatua kwa mfumo wa Wanachama, tuna vingi vya kutukwamisha, ikiwemo kulipia tu kadi
Watapita na kwenda zao, watatuacha na ubishi wetu
30/11/2025
Bush stars... Nitajie majina ya kila mchezaji wa hiki kikosi
30/11/2025
MRISHO KHALFAN NGASSA 'SHIBOBO MASTER', UKISTAAJABU YA M***A UTAYAONA YA MWANA WA HAWA
Nakumbuka sana Mafundisho ya Dini, kile kisa cha Adam na Hawa (Mwanamke) alimshawishi Adam wale tunda la kati, matokeo yake ikawa mateso ila anguko hilo lilikuwa ni hatua muhimu katika maku*i ya Binadamu
Kutokana na anguko lile Mungu aliwaleta Manabii ikiwemo Massih Issa Bin Mariam, walikuja kulipia makosa ya binadamu kwa sharti ya toba, lakini bado kuna vitu vitasalia na mshangao mkubwa sana duniani
Wapo wapi watu wale walioshuhudia Mwanamke akilia kwa furaha na anaweza pia kucheka kwa huzuni, wapo wapi watu wale waliowahi kushuhudia akiacha mbachao kwa msala upitao, wapo wapi watu wale
Bado sijashangazwa sana na yote hapo juu, ila mshangao wangu ni maeneo ya ziwa lilopewa jina na Explorer John Hanning Speke 1858, aliliita Victoria kutokana na jina la Malkia wa Uingereza, hapo ndipo stori yangu inaanzia
Historia yetu inaanzia kwa Mzee Khalfan Ngassa 'Babu' nyota wa zamani wa Pamba 'TP Lindanda', alietamba 1991 kwenye u*i wa Simba akisimama k**a Kiungo aliipa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati, anafanya maajabu mbele ya Ramadhan Lenny, Idi Kibode, Bakari Iddi na Method Mogela
1991 hiyo Mzee anatamba, nyuma yake ana kichanga cha miaka miwili, Mrisho aliyezaliwa 1989, kirusi kingine cha mpira alochokileta kuendeleza jina lake, wakati Mzee anapokezana pass na Ally Bushiri, Kitwana Seleman, Hamza Mponda, Fumo Felician pale Lindanda, lakini kwenye nyumba moja Mama Mrisho anakilea kichanga
Judith Wambura 'Lady Jaydee' aliimba siku hazigandi, ikawa usiku na ikawa mchana, watoto wadogo pale Kirumba walianza kuhisi joto la jiwe na mpira sukari wa Mtoto wa Khalfan, nae ni Mrisho Ngassa, mbele ya Kelvin Yondan, Jerry Tegete na Henry Joseph Shindika
Hakuna aliewajali sana ila ni Toto Africans 'Wanakesha Mapanda' walitengeneza mzinga kwa ajili ya kufaidi asali ya nyuki wale, Haukuwepo Msomaji ila Malaika wako walikuwepo, kila mtu alipita njia yake kwa watoto wale wa Mtaa, ila Mrisho alielekea Kagera Sugar
Mrisho alikuwepo kikosi cha Serengeti Boys kile kilichofuzu Mataifa ya Afrika 2005, japo CAF waliwaondoa kwa sakata la umri wa Nurdin Bakari
Itaendelea
28/11/2025
Binadamu hawa wawili walikua wanaupiga mzigo kimya kimya, ni k**a yai bovu lililovishwa shuka, ni kazi kujua wanafanya nini uwanjani ila ulikua unaona mpira unahama kila sehemu😊
Lionel Messi ni gari moja lililokaa Parking na kuvutia sana, ila nyuma ya abiria aliokuwa anawaendesha kulikua na haya matairi ya mbele, kwenye hilo gari hilo, walikua wanaonesha muelekeo wa gari la Barcelona
Ukisikia Barcelona wanauza binadamu hawa wawili ingekua sio barani Ulaya, hawakua tayari kushuhudia hii miguu minne inapatikana tena Ulaya, watu walikua tayari kuvunja vibubu ku*ipata huduma hizo, ila moja ilienda Japan na moja ikaenda Qatar
Wewe unawaita viungo mimi nawaita grisi kwenye vyuma, nawaita nyundo pale Mahak**ani, nawaita sabuni ya roho kwa wapenzi wa soka, waliufanya mchezo wa soka uwe rahisi na kutazamika machoni, ilikua inaruhusiwa hata mtoto aliyezaliwa siku mbili zilitopita kutazama soka lao
Huku Hispania wale Traffic wakisimamisha ndinga zao walikua wanawaomba radhi kwa foleni, kisha hupiga picha na kwenda kuvimba Instagram, "NIKIWA NA INIESTA" "NIKIWA NA XAVI" ilikua sio rahisi kuwaruhusu wapite bila kula nao picha, haikuwa rahisi
Hakikisha ukipanda gari lao umefunga mkanda, k**a unacheza nao unaweza kuwa jicho nyanya usione wapi wanapeleka mpira, muulize Sir Alex Ferguson pale Wembley alitetemeka, Xavi peke yake aligonga pass kuliko United yote, Iniesta alikua k**a Hi**er mbele ya dimba, pass za mamlaka na maamu*i shupavu
Binadamu wachache kuwahi kutokea na kuufanya mchezo wa soka uwe rahisi, walikuja kubadili akili ya Eusebio kwenye kiungo pale Nou Camp, walikua duplicate ya Zinadine Zidane, walikua version tofauti na wakina Simeone walivyotafsiri kiungo, walikua binadamu wa aina yao peke yako😊
Guardiola aliaminiwa sana na Johann Cruyff, alitamani sana mtu acheze 4-3-3 aliyowaza kichwani mwake, Guardiola akaja kufaulu nayo akiwa Kocha chini ya Binadamu hawa, k**a sheli walikua full tank🙌
Asanteni kwa kumbukumbu Xavi Hernandez La Macquiao na Don Andres Iniesta Lujan
22/11/2025
YANGA AFRIKA, PENYE NG'OMBE HAPAKOSI MMASAI
Diego Maradona katikati mwa uwanja pale Camp Nou, anamchukua Kiungo wa Deportivo kisha anamvesha kanzu Kiungo mwingine, anakusanya mabeki na kuweka kambani ila hashangilii bao
Moyoni mwake tu anajiona hafai kucheza kwenye Klabu ambayo yeye anahisi haina deni kwake, aliwakumbuka Wananchi wa Boca Juniors pale La Bombonera, alicheza kwakuwa alikuwa na deni kubwa kwao
Baada ya mchezo akamwambia Wakala wake, nitafutie timu Ulaya k**a Boca, k**a haipo naomba nirudi nyumbani Argentina nikacheze mbele ya watu wangu, wakala alipambana mpaka wakahamia Napoli, Wananchi wengine Kusini mwa Italia
Niliwahi kuandika kitu kuhusu timu zote za Wananchi duniani kote, niliwahi kusema kitu kuwa uvaapo jezi zao una deni kubwa kwao, hawana pesa ya kukulipa mshahara wako, hawana Maisha ya kukugharamia ila wanachoweza ni kusimama nyuma yako kwa Muda wote
Kumradhi kwa kukupeleka Argentina kisha Hispania na Italia, naomba nikulete makutano ya Twiga na Jangwani, shukrani zangu za dhati ni kwa Mpiga Picha wa Yanga Afrika, kanipa picha tatu za maana halisi ya timu ya Wananchi
Picha ya kwanza kutoka kmc complex pale mwenge , Mwananchi mmoja Kijana tu kavua jezi yake na kuipeperusha, huenda hana maisha k**a Rostam Aziz, miamala kam GSM wala fedha k**a za Dewji ila nikuhakikishie ana furaha kubwa kuliko wao, timu yake hii na damu yake hii
Picha ya pili ni Mama na Mwanae, sahau kuhusu foleni ya Dar Es Salaam, sahau huenda hana gari binafsi ila kipi kina nguvu kwake zaidi ya kumbeba Mwanae, kuvaa jezi ya Mwananchi na kujibana asisuke ili aende Taifa, nikuhakikishie ana furaha kuliko Nandy, Zuchu wala Ruby, timu yake hii
Picha ya mwisho ni Mzee wetu, katikati ya vijana kasimama yeye! Kuwarithisha kizazi cha wakina Sunday Manara, Salum Kabunda na sasa wakina pacome zouzou, katika furaha yake kubwa ya uhai ni kupata pia kuiona Yanga Afrika, ndio maana halisi ya Wananchi
Basi popote umwonapo ng'ombe hapakosi Mmasai, Wananchi ni ngome kongwe, hakuna alietawala vichwa vyao bali timu imetawala mioyo yao.. All the best huko zanzibar wananchi mwarabu afe leo
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Website
Address
Sabasaba
Iringa