Beka mambo

Beka mambo

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Beka mambo, Sports, Kibaha.

03/08/2022

TETESI ZA MASTAA TANZANIA
Na Kastul Elias

Mshambuliaji Nelson Okwa(28) raia wa Nigeria🇳🇬 anatajwa kuingia nchini Tanzania usiku wa leo kukamilisha dili lake la kujiunga na Simba SC 🇹🇿.
Simba SC imepanga kumtambulisha nyota huyo katika kilele cha Simba Day itakayofanyika Agosti 8 mwaka huu.

Baada ya kukaa nchini kwa takribani siku Siku saba sasa, tetesi zinadai wakala wa wachezaji raia wa DR Congo 🇨🇩 Faustine Mukandila anatajwa kumalizana na Yanga SC🇹🇿 juu ya uhamisho wa mchezaji Fabrice Ngoma ambaye mpaka sasa hana timu baada ya kuachana na Wydad AC ya nchini Morocco.
K**a dili litakamilika Ngoma atajiunga na Yanga SC katika dirisha dogo la usajili.

Kocha wa Azam FC, Abdihamid Moallin amesema ana imani na beki kinda wa timu hiyo, Twaribu Nuru(18).
Moallin amesisitiza kuwa Twarib atakuja kuwa beki tegemeo katika kikosi cha Taifa Stars.

Aliyekuwa beki wa Azam FC Nicolas Wadada🇺🇬 amejiunga na Ihefu FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Namungo FC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Pius Buswita🇹🇿 kutoka Ruvu Shooting Stars.

Polisi Tanzania imethibitisha kumsajili mchezaji Idd Kipagwile🇹🇿 kutoka Azam FC.

Ihefu FC🇹🇿 imetangaza kukamilisha usajili wa FC mshambuliaji Never Tigere kutoka Azam FC.

Aliyekuwa golikipa wa Geita Gold FC, Khomein Abubakar amejiunga na Singida Big Stars akitokea Geita Gold FC.

07/12/2019

Kila jambo na wakat wake 👆

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Kibaha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Kibaha