Apostle Israel And Ruthu Rehobothi

Apostle Israel And Ruthu Rehobothi

Share

Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo Huduma za Kiroho

10/01/2024

Jifunze kufanya mambo mapya ambayo hujawai kuyafanya
Maisha ni mapambano yasiyoshirikisha visu na mapanga nooo

Unapoiona fursa ama kuambiwa habari za fursa na ukaikimbilia na kuifanyia kazi bila kuchoka hayo ndiyo mapambano ....

Maskini wengi wanaongoza kuuliza nani kafanikiwa .....maana yake unaskini wao umesababishwa na kuwa tegemezi pia Hawa ni Tomaso kwa majina halisi, inatabiriwa kuwa hata kuuona ufalme wa mbinguni siyo rahisi sana😎👇🏻

Kwa sababu hawawezi kuamini pasipo kuona sasa Mungu wetu mtukufu haonekani ✍🏻✍🏻 maana yake hapo ni kwamba hawa ndugu zetu hawaamini kwamba mungu yupo - *Tomaso*

27/12/2023

MATOFALI 10 YA NDOA BORA!!

1.Lazima Ujue Kwamba Wewe Ni MKE Na Ni Wajibu Wako KUSHUKA NA KUMTII MUMEO
“Enyi Wake Watiini Waume Zenu K**a Kutaniko Linavyomtii Kristo Yesu”

2.Lazima Ujue Kwamba MUMEO NI KIONGOZI WAKO, Haijalishi Uko SMART KIASI GANI, Mume Anabaki Kuwa Mume… Hata Ukiwa Rais Wa Nchi, Ukirudi Nyumbani UNAKUWA MKE WA MTU; Hapo Elimu, Nafasi, Cheo, Umaarufu Havifanyi Kazi.
“Mume Ni Kichwa Cha Mkewe… Hata K**a Kichwa Hakina Akili Bado Ni Kichwa, Na Unadhirisha Usivyo Na Akili Zaidi Kwa Kukubali Kuolewa Na Mjinga… Umeshaolewa, Umegundua Ni Mjinga, Ishi Naye Kwa Akili Na Msaidie Kujua Nafasi Yake Na Muache Akae Kwenye Nafasi Yake”

3.Usiwe Mjinga Kiasi Cha Kutoka Nje Kwenda Kueleza Mapungufu Ya Mumeo; Midomo Ya Wanawake Wengi Imevunja Ndoa Zao… Hao Mashoga, Marafiki, Ndugu Zako Watakusikiliza Ila Hawatatatua Shida Zako Bali Watachangia Kuibomoa.
“Mwanamke Mpumbavu Huibomoa Nyumba Yake Kwa Mikono Yake Mwenyewe”

4.Simama Kidete Na Umlinde Mumeo Anaposhambuliwa… Chako Ni Chako Hata K**a Kina Mapungufu… Mtetee Mumeo Mbele Za Watu Na mkosoe Mnapokuwa WAWILI CHUMBANI.
“Naye Abigaili Akamwangukia Daudi Akamfichia Mumewe Aibu Na Kumlinda Asiuawe”

5.Mumeo Akitoka Nje Ya Ndoa Kutafuta Nyumba Ndogo, Kabla Ya Kutafuta Pepo Aliyemwingia, Tafuta Mlango Ambao Huyo Pepo Ameutumia… Inawezekana Ulipokuwa Single Ulikuwa UNAJIPENDA, Unapiga PAMBA MPAKA BASI, Umeolewa UNAJIVALIA KIVYOVYOTE [shauri Yako]; Inawezekana Ulipokuwa Hujampata LUGHA YAKO ILIKUWA SUPER, Lakini Sasa Unajibu Unavyojisikia [Shauri Yako]; Inawezekana Ulipokuwa Hujavaa Pete ULIKUWA UNAWAPENDA NA KUWATHAMINI NDUGU NA WAZAZI WAKE, Lakini Ulipoingia Tu, Ndio Umeona KARAHA YA MAWIFI NA NDUGU WA MUME [shauri yako]… INAWEZEKANA NI KITANDANI [Biblia Inasema MKE HANA UMILIKI JUU YA MWILI WAKE ISIPOKUWA MUMEWE] Usisahau Hii Ni Ya Muhimu Sana, UKISEMA ANAKUCHOSHA “KWA KUKUJIA MARA KWA MARA” [Shauri Yako]!
“Mungu amefanya jambo jipya duniani ya kwamba MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME”

6.Usisahau Kwamba Ni Wajibu Wa Mke KUAMKA KABLA USIKU HAUJAISHA NA KUPIGA KAZI ZOTE ZA MUHIMU NDANI… Biblia Imesema Hili, MITHALI 31 [BIBLIA HAISEMI NI KAZI YA HOUSE GIRL; UKIMPA HOUSE GIRL AZIPIGE UMEMPA NAFASI YA KUWA MKE BADALA YAKE, MAANA NI KAZI ZA MKE MWEMA HIZI]
“Mke Mwema Huamka Kabla Usiku Haujaisha Ili Kuweka Sawa Mambo Ya Nyumbani Mwake Kwa Siku Inayoanza Baada Ya Usiku Huo”

7.Ni Lazima MKE AWE NA KITU CHA KUFANYA… Ukiwa tu GOLIKIPA, Hakuna VIUNGO Wala MABEKI Kukulinda UTAFUNGWA MAGOLI.
Mke Ambaye ANA AKILI NZURI Lazima AWE NA KITU CHA KUINGIZA KIPATO…Afanye Kazi Kwa Mikono Yake Mwenyewe, Na Kutunza Watu Wa Nyumbani Kwake, MITHALI 31 IKO WAZI K**A UNATAKA NDOA YAKO ISIMAME, UKIKWEPA IMEKULA KWAKO!
“Mke Mwema Hufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kuwapa chakula watu wa nyumbani kwake”

8.Mke Mwenye Hekima ANAULINDA UHUSIANO NA MAMA MKWE [Hii Ni Zawadi Ya Pekee Kwa Mumeo], Moyo Wa mtoto Wa Kiume Humpenda Na Kumjali Mama, Usisahau Hii Itakusaidia, NI SILAHA MUHIMU YA VITA!
SOMA KITABU CHA RUTHU Utaona Ruthu Alivyocheza Kete Zake Vizuri Na Kuuteka Moyo Wa Mama Mkwe.
“Mke Mwenye Busara Huhakikisha Anauteka Moyo Wa Mumewe Kwa Kuwa Kipenzi Cha Mama Mkwe”

9.Mke Mwenye Busara Anajua Ya Kwamba Ni Jambo Moja Kuwa Mzazi [Mwanamke Aliyezaa] Na Ni Jambo Jingine Kuwa MAMA.
Kuzaa Ni Kuporomosha Kiumbe Baada Ya Miezi 9 Aliyoweka Mungu Lakini Kuwa Mama Kunategemea MALEZI SAHIHI NA BORA Yatakayoweka Msingi Mwema Na Bora Usiofutika Kwa Mwanao.
“Mke Mwema Humlea Mtoto Wake Katika Njia Impasayo Ambayo Hataiacha Hata Atakapokuwa Mzee”

10.Mke Mwenye Hekima HUUWEKA MOYO WAKE KWA MUNGU: Huku Ndiko Anakoeleza Mapungufu Yake, Mapungufu Ya Mume Wake, Na Kukabidhi Ndoa Yao KWENYE MIKONO SALAMA NA MAKINI YA MUNGU. Mungu Anaweza Kubadili Chochote Ambacho Wazazi, Washenga Au Washauri Wa Ndoa Hawawezi Kugeuza Au Kutatua.
“Mke Mwema Hufunga Na Kuomba Kwa Ajili Ya Mumewe, Ndoa Na Familia Yake… Ni Rafiki Wa Uwepo Wa Mungu”

09/12/2023

Mwanamke nikukumbushe k**a umezaa una watoto jukumu la kulea haliishii tu kwa mtoto wa k**e jukumu la maombi si juu ya mtoto wa k**e pekee.

Jukumu la malezi na maombi linawahusu watoto wa kiume pia hawa watoto wanahitaji msaada mkubwa wa wazazi wanahitaji ukaribu wa wazazi ili wakueleze changamoto wanazopitia wazazi tuwasaidie kuzitatua.

Mtoto wa kiume pia anazo changamoto si mtu wa kukemewa tu bali mfanye rafiki akueleze mahali anapitia ili umshauri na kumuombea pia.

Dunia ya utandawazi hii mtoto wa kiume pia anaweza kujiingiza kwenye uzinzi akiwa na umri mdogo miaka 17+ si kwasababu amependa ila shetani yupo kazini ndugu zangu watoto wa k**e nao wanatongoza tena wananyosha mistari hiyooo utaipenda.

K**a hujajua kukaa na mtoto wako wa kiume hujui kuomba kwaajili yake aise.

Mama jukumu la kulea haliishi kwako hadi pale Mungu amempa mwenzi wake kwa msaada wa maombi yako hapo ndipo kuna mipaka yako mzazi.

Mungu akupe neema ya kubeba mzigo wa maombi kwaajili ya watoto wako usiwalee bora liende ipo siku utakuja kujutia sana.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Uyole
Mbeya