abbi madboe

abbi madboe

Share

Football ⚽ for everyone best enjoyment is football ⚽⚽

07/09/2024

07/09/2024

Watu 12 wakiwemo Watoto wawili wamefariki na wengine 36 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya, ajali hiyo imetokea leo ljumaa September 06,2024, baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameiambia kuwa “Basi liliacha njia kwenye kona kali kwenye mteremko mkali na kugonga gema na kupinduka na kusababisha vifo vya Watu 12 (Wanaume watano, Wanawake 7) miongoni mwao Watoto wadogo wawili, na kusababisha majeruhi ya Watu zaidi ya 36 ambao wenye hali mbaya ni watano”

“Kuna Watoto wameachwa mpaka sasa hivi Wazazi wao wamefariki, ni Watoto wa miezi sita hadi miezi nane, tunaendelea kufanya mawasiliano na Ndugu wa Marehemu maeneo ya Tabora, Mbeya na maeneo mengine kwasababu kote kuna Watu ambao walikuwa wanasafiri”

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi, Dereva alianza kwa kasi kubwa akitokea Mbeya kwenda Tabora alipita kona zote ngumungumu kabla hajafika kona ngumu ya mwisho mizigo ikaanza kudondoka kwenye gari baada ya buti ya gari kufunguka, Kijana mmoja ambaye sasa ni Marehemu akatoa taarifa mizigo inaanguka, gari likasimama wakapakia mizigo”

“Wakiwa pale mabasi mawili yakawapita yakiwa yanaenda Tabora huwa wanakimbizana njiani kutafuta abiria, kwahiyo alipomaliza kupakia akaanza kukimbia tena kufika kwenye kona gari ikamshinda bampa la juu likakatika ikaanza kuwaburuza vichwa vikawa vinaburuzika”

Want your business to be the top-listed Photography Service in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Soweto
Mbeya
MBEYATOWN