MAZAO
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from MAZAO, Business service, Mbalizi, Mbeya.
FAIDA ZA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA
Umewahi kula Maboga? K**a jibu ni ndio basi utakuwa unajua utamu na upekee wa chakula hiki. Ni moja ya chakula maarufu na kinachopendwa zaidi katika jamii za kiafrika ikiwemo Tanzania. Mbali na kutumiwa k**a chakula je wajua maboga hutumika k**a dawa? Mbegu za maboga ndio hasa fahari ya uwezo wa maboga kutibu ilipokaa.
Mbali na mbegu za maboga lakini pia majani na tunda lenyewe pia zina faida lukuki za kiafya. Kisayansi maboga hutambuliwa kwa jina la Cucurbita pepo. Mmea huu unalimwa sehemu zote za ulimwengu ikiwemo Tanzania.
Matumizi ya maboga na sehemu zake k**a chakula hutofautiana kulingana na maeneo mbalimbali. Kuna jamii ambazo hutumia maboga k**a mboga, k**a chakula rasmi na pia hutumiwa k**a kiambata cha kutengenezea pombe.
MBEGU ZA MABOGA ZINA NINI NDANI YAKE?
Maboga yana faida nyingi za kiafya kutokana na uwepo wa kemikali nyingi za kibaolojia ndani ya mmea huu. Baadhi ya kemikali hizo ni Wanga, protini, madini joto, mafuta, sterols, protini na para-aminobenzoic acid.
Tunda au boga lenyewe lina kiwango kikubwa cha kemikali tiba za carotenoids, d-chiro-Inositol na para-aminobenzoic acid.
Wakati mbegu za maboga zina kemikali tiba za mafuta(linoleic acid na oleic acid), protini, sterols, cucurbitin, vitamini E, beta-carotene na madini joto ya iron(chuma), zinc na selenium.
Kemikali za sterols.
Ni kundi la kemikali ambalo hutengenezwa na mimea na kuhifadhiwa zaidi katika mbegu na mafuta ya mmea. Kemikali hii ina faida nyingi za kiafya zikiwemo kupunguza kiwango cha rehemu hatari mwilini, kutibu maradhi ya kansa ya mfumo wa chakula na pia kusaidia kupunguza matatizo ya mfumo wa mzunguko wa damu.
Kemikali ya Cucurbitin.
Hii hupatikana katika mbegu za maboga na tafiti zinaonyesha kemikali hii huangamiza minyoo na pia ni kiantioksideshaji kikubwa.
FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA NI ZIPI?
Zifuatazo ni faida za mbegu za maboga.
1-Kuua na kuangamiza minyoo.
Mbegu za maboga husaidia kuangamiza na kuua vimelea vya minyoo kutokana na uwepo wa kemikali ya cucurbitin. Matumizi ya mbegu za maboga yanashauriwa zaidi kwa Watoto na wajawazito kutokana sababu kwamba ni kundi linalohitaji tiba salama zaidi.
2-Kutibu na Kusaidia nafuu ya uvimbe wa tezi dume.
Mbegu za maboga husaidia kutibu na kuleta nafuu kwa wagonjwa wa uvimbe wa tezi dume. Hii inatokana na uwepo wa kemikali za sterols ambazo husaidia kuleta mlinganyo wa homoni.
3-Vilevile sterols na kemikali nyinginezo ndani ya mbegu za maboga husaidia kuondoa uvimbe ndani ya tezi dume na sehemu nvinginezo za mwili.
4-Hutumiwa k**a lishe maalumu.
Mbegu za maboga hutumiwa k**a tiba kwa watu wenye upungufu wa madini joto ya zink, selenium na iron, kwa vile madini haya yapo kwa kiwango kikubwa ndani ya mbegu hizi.
5-Kutibu na tatizo la sonona au msongo wa mawazo.
Mbegu za maboga hutumiwa katika kutibu tatizo la msongo wa mawazo kutokana na uwepo wa kemikali ya L-tryptophan. Kemikali hii husaidia uzalishwaji wa homoni za serotonin katika ubongo ambazo huusika na furaha.
6-Kutibu maradhi ya bakteria na fangasi.
Uwepo wa kemikali za α-moschin na β-moschin ndani ya mbegu za maboga kunazipa uwezo wa kupambana na fangasi na bakteria wa aina mbalimbali mwilini.
7-Kukulinda na maradhi ya saratani.
Mbegu za maboga na boga lenyewe vina kiwango kikubwa cha kemikali za carotenoids ambazo huulinda mwili dhidi ya saratani hasa saratani ya mfumo wa chakula k**a vile saratani ya utumbo mpana.
8-Huondoa sumu mwilini.
Mbegu za maboga zina kiwango kikubwa cha vitamini E. Vitamin E husaidia kuondoa chaji huru mwilini ambazo ni hatari kwa uhai wa seli. Uwepo wa chaji huru ndani ya mwili kunaua seli za mwili nakupunguza uwezo wa mwili kukabiliana na maradhi mbalimbali k**a vile saratani na kisukari.
9-Kutibu maradhi ya kisukali.
d-chiro-Inositol ndani ya mbegu za maboga husaidia utendaji kazi wa kemikali ya insulin ndani ya mwili. Insulin ni moja ya kemikali/homoni inayohusika na kurekebisha sukari ya mwili.
10-Kusaidia ukuaji bora wa ubongo.
Kwa mtoto mbegu za maboga zina zaidi ya faida za kiafya kwa vile zina kiwango kikubwa cha zinc, madini joto hay ani muhimu zaidi katika ukuaji wa ubongo.
Namna ya kutumia mbegu za maboga k**a tiba.
Mbali na mbegu, majani na tunda/boga vyote huweza kutumika k**a tiba. Mbegu za maboga huweza kutumiwa kwa kutafuna zikiwa mbichi, zimechemshwa au kukaangwa. Lakini pia zinaweza kutumiwa katika namna ya unga.
Pia unaweza kunufaika na faida za mbegu za maboga kwa kutumia mafuta yatokanayo na mbegu hizo. Mafuta ya mbegu za maboga yana kemikali sawa na zile zinazopatikana katika mbegu na huweza kutumiwa kwa kupaka pia.
Tumia mbegu za maboga kwa wingi iwezekanavyo.
Tumia unga wa mbegu za maboga k**a sehemu ya lishe kwa chakula cha mtoto wako.
Mafuta ya mbegu za maboga yanaweza kuwa hatari kwako, tumia kwa uangalifu na kwa maelezo na maelekezo ya kitaalamu.
Nandomana Chewa Products. Imeamua kuja na bites zenye tiba asili ndani ake apa tunazungumzia BOGA PLUS,bidhaa yenye mchanganyiko wa Bisi karanga za kukaanga pamoja na mbegu za maboga.
Kumbuka:
Unaweza kula mahala popote pale na vyote vipo katika kifungashio kimoja.
Kwa mawasiliano:
0759021203/067837865
Instagram:Products.Chewa
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Mbalizi
Mbeya
53208