Isaiah The JUDGE

Isaiah The JUDGE

Share

A MAN ON HIS TIME! APOSTLE OF JESUS CHRIST
ASS-PASTOR AT @ABC Global-Mbagala Mission

27/02/2026

BIDII HUFANYA MTU AWE MTAWALA (Mithali 12:24)

Siku zote kwenye maisha, ukiruhusu tu mtu akupite bidii basi umeruhusu huyo mtu awe mkuu juu yako na akutawale.

Huwezi kuwa mkuu au mtawala ikiwa unalala sawa na wao, unafanya k**a wao! Lazima uwe na jambo la ziada (bidii ya ziada).

Jinoe wakiwa usingizini, na fanya kazi wakiwa wanapumzika, na zaidi ya yote ongeza ubora uliokosekana kwa wote mpaka thamani yako isizuilike!

Huwezi kuwa na ukuu au mamlaka ya kutawala zaidi ya bidii uliyo nayo. Watu wenye bidii ni watu wakuu! Watu wenye bidii huwa ni watawala!

Huhitaji cheo au title (jina) fulani ili uwe mtawala, unahitaji bidii kwanza ili uwe mtawala. Hakuna bidii inayomwacha mtu kwenye kundi la ukawaida! Kila bidii humvuta na kumsukuma mtu juu kwenye ukuu bila kujali jinsia, rangi, umri, au historia aliyo nayo.

Mithali 12:24 "mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi."

Je, wewe una bidii? Basi k**a huna bidii kubali kulipishwa kodi!

Dah! Kumbe maisha ya uvivu yana gharama kubwa zaidi kuliko hata maisha ya bidii!

Usisubiri cheo cha kupewa, Lipa gharama uwe MKUU.

Shalom!
Pastor Isaiah Imani.
27 February 2026

13/12/2025

SUALA LA UNAOLEWA NA NANI?
Katika mambo muhimu ya mwanamke kuzingatia, ni suala la unaolewa na nani.

Zipo sifa nyingi za mwanaume zinazopendekezwa na Neno la Mungu ambazo Kila mmoja anapaswa kuzizingatia katika kuchagua nani wa kuambatana naye.

Unahitaji mwanaume ambaye umejihakikishia kuwa utamuamini bila mashaka, Kwa Sababu una uhakika na

Moja Mahusiano yake mazuri na Mungu wa kweli, (Mahusiano na Mungu ndio MSINGI WA mahusiano mengine yote). Ubora WA mahusiano ya MTU na MTU hutegemea Hali yake ya kiroho (Yaani mahusiano yake na Mungu)

Pili Mahusiano mazuri na mamlaka halali zilizo juu yake k**a vile wazazi na walezi wa kiroho, na wa kimwili na mamlaka zake zingine,

Tatu mahusiano yake mazuri na kusudi la kuumbwa kwake pamoja na maono ya Mungu aliyo nayo ndani yake na anayoyafanyia kazi.

Nje na hayo mambo matatu uwe na uhakika utaangukia kwenye mikono ya Nabali na utaonekana pia huna akili hata k**a wewe ni Abigaili mwenye akili.

Sara alimtii mume wake Kwa Sababu alijua wazi kuwa , Ibrahimu anamjua Mungu, analokusudi la Mungu, lakini pia ni mtii Kwa mamlaka halali na alikuwa chini ya malezi ya kiroho ya Kuhani melkizedeki.

Sasa, sisemi usimtii mume wako Kwa Sababu Hana hivyo vigezo, haswa k**a ulishaolewa naye! Ni wajibu wako kumtii Labda unachoweza zaidi ni Kumwombea Mungu ambadilishe na kumwokoa Kwa Neema yake.

Lakini Kwa Binti ambaye hajaolewa bado usithubutu kabisa kujiingiza kwenye agano la ndoa na MTU ambaye unajua kabisa hutaweza kumtii Kwa Sababu huna uhakika na vigezo nilivyotaja hapo juu! Wazungu wanasema (ga) Usijaribie hii kwako (Don't try this at home) utajuta mno.

Maandiko yanatwambia wazi kabisa usifungiwe nira pamoja na MTU asiyeamini Kwa jinsi isivyo sawasawa. Maana yake HUPASWI kumwamini yeyote asiyemwamini Yesu na kumfuata Kwa dhati. (2 Wakorintho 6:14-18)

Kichwa cha mwanamke ni mumewe na kichwa cha mume ni Yesu Kristo, kuolewa na asiyemwamini Yesu ni sawa na kuwa na MTU mwenye kichwa cha shetani maana hakuna anayeweza kuwa bila Yesu halafu akabaki bila shetani.

Ukiolewa na asiyeamini ujue umeshajiuza chini ya mamlaka ya shetani.

Usijidanganye kabisa kwamba huyu mtu Mbona ni mwema, au Mbona ni mpole, au ni Bora kuliko hata waliookoka! Lazima ujue wazi unajirahisishia safari Yako kwenda jehanamu!

Mtu mmoja aliwahi kusema "When you marry wrong heaven become probability and hell become a possibility" akimaanisha ulikosea ndoa basi kuingia mbinguni ni bahati lakini jehanamu ni uwezekano mkubwa.

Lo! Utashangazwa, huyo asiye na Yesu ndani yake, anaweza kuingiwa na shetani muda wowote na akakufanyia mambo ya kishetani au kukupa maelekezo ya kishetani Ili akukwamishe kwenye mahusiano yako na Mungu, mahusiano yako na kusudi au maono uliyo nayo, Mahusiano Yako na watu wako muhimu, pamoja na mahusiano Yako na wewe mwenye (ukajikuta Kila siku unaishi kwenye maumivu na migogoro ya ndani isiyoisha).

Yuda Isikarioti hakuwa mcha Mungu wa kweli ingawa alikuwa mwanadini mzuri na mshirika mwaminifu wa YESU, lakini Kwa Sababu ya kutokuwa na mahusiano ya kina na Mungu Shetani alipata nafasi ya kumtumia kwaajili ya AJENDA zake za kigiza za kumsaliti Yesu.

Ndiyo maana si ajabu unahusiana na mwanaume ambaye Kila siku anakutaka ufanye ngono kabla ya ndoa na unadhani Uko na MTU sahihi, au anakuzungumzisha mambo ya hovyo, anakuomba picha za uchi, anakushikashika k**a mkewe! Halafu wewe unadhani huyo ni MTU sahihi.

Hakikisha mume wako ni tegemezi Kwa maelekezo ya Mungu Ili asije akakuagiza kufanya vitu kinyume na Mungu.

Hakikisha mwanaume anaongozwa na amejitiisha haswa Kwa Mamlaka ya Neno la Mungu.

Shalom, Nawapenda mno 🥰
[Pastor Isaiah Imani]

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Mbalizi
Mbeya