Japhet Katana
Empowering Lives Through the Gospel Of Jesus Christ. Building Faith, Transforming Hearts, and Revealing God’s Unfailing Love. Kindly Welcome.
❤️
20/12/2025
ZINGATIA MAMBO HAYA MUHIMU UNAPOTEMBELEA WAHITAJI:
1. Fanya utafiti kujua mahitaji yao kabla ya kuwaendea.
2. Tatua matatizo yao ya muda mrefu hata kwa sehemu ukiwa na uwezo.
3. Acha keshi kidogo kwaajili ya mahitaji ya wahudumu wa kituo.
4. Si lazima upeleke vitu wakati mwingine wanahitaji msaada wa nguvu kazi wasaidie au wape ujuzi au kipawa chako
5. Sema nao neno la faraja na kuwatia moyo
Ukihitaji msaada wa kufahamu baadhi ya vituo ambavyo tumevifikia kwa matendo ya upendo au unataka kuwa unashiriki nasi tuwasiliane kwa namba zangu hapa chini.
Mawasiliano zaidi:
+255745746691
Japhet Katana
19/11/2025
SI JAMAA ALISEMA ANA DAMU YA KUNGURU‼️
Katika moja ya simu nilipokea jana kwa bashasha na hamu kubwa kutaka kusikia yaliyojili ni hii, maana aliyepiga simu hii ni rafiki yangu sana..
Baada ya salamu kwa sekunde chache akaanza kunipa kisa kizima, si unamkumbuka yule jamaa kicheche alikuwa akiruka na mabinti lukuki? Mimi nikawa nauliza yupi huyo tena? anajibu yaani namaanisha yule jamaa kila unapokutana naye ni stori za mademu mara yule binti kisu mkali wa mtaa, Mimi nishatoka naye. Huku usoni anajawa na tabasamu kubwa akitaka kuonyesha k**a anafaiidi kwa matendo yake hayo na kuonyesha k**a ni mwanaume kweli kweli. Huku ukijaribu kumwonya juu ya mwenendo wake huo anawahi kusema "kumbe hujui mimi nina damu ya kunguru" Sasa Mimi nakupata si ungesema tuu yule Damu ya kunguru.. lakini yule tumemwonya mara nyingi sana lakini amekuwa sikio la kufa zaidi anatia pamba masikioni. unakumbuka mara ya mwisho tumemwambia damu yake hiyo iko siku itakuwa k**a ya kunguni? yes nakumbuka..
Mimi binafsi nikapata shauku ya kujua hiyo damu ya Kunguru ni damu ya jinsi gani? baada ya kuumiza kichwa na kuuliza watu wa mtaani ndipo nikajua kumbe anaposema ana damu ya Kunguru inamaana ana damu ya group "O" damu ya aina hii inaaminika ni ngumu kuchukua vimelea vya magonjwa au kuambukizwa magonjwa. pamoja na hayo bado tukawa tunamshauri kuwa unaweza usipate magonjwa kwa sababu ya damu yako k**a unavyosema, Kwa kebehi anaongezea kuwa anatumia mipira. Tunapokaza kumuuliza na dhambi je, unakinga na nini isikupate kwa matendo hayo machafu? maana ni amri ya Mungu kuwa Usizini.
Majibu yake ya mizaha na kusema haamini k**a inawezekana mtu kuishi hivi hivi. anazo sababu lukuki za wanasayansi anaaamini hawezi kuwa vizuri k**a hashiriki katika mambo yahusianayo na ngono. Anasingizia mara ooh sisi vijana damu zinachemka mara kufanya hivi nabadili oili, tunamwambia wewe si gari mpaka ubadili hizo oili lakini amekuwa akikaza shingo yake. Akisema nitaokoka lakini si sasa nitaokoka uzeeni sasa nile ujana kwanza. Tunaendelea kumpa majibu ya hoja ili abadilike, kuwa kwani wangapi vijana wameondoka hata bila kuzeeka wengine kiumri wadogo kuliko wewe unapaswa kubadilika sasa uokoke na umpokee Bwana Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako binafsi utashinda tamaa na kutumikishwa na dhambi nawe uwe huru k**a sisi. Anatamani lakini anatafakari kwa muda akiwa ameinamisha kichwa chini. Anasema lakini kweli mnachosema lakini nawaza naona k**a mimi sitaweza.. tunamwambia mwenyewe huwezi lakini ukiamini unapokea nguvu ya Roho Mtakatifu inakusaidia kuweza mwili wako na kuishinda dhambi inatusaidia wenzio pia. anawaza anasema nitaamua na mimi siku Moja..
Basi sasa juzi bwana eeh! si kaumwa ugonjwa ambao umemfanya kukiri na kuelewa yote tuliyokuwa tunamweleza ili abadilike. kuwa unayofanya huko sirini siku moja yatakuwa peupe. Si jamaa alikuwa anasema ana damu ya kunguru! Sasa yalipomfika ya mchozi na haja ndogo zikawa zinakwenda pamoja huku moyoni amejaa majuto na simanzi pesa zake zote katumia katika uzinzi kuharibu mabinti amekuwa kero hata wazazi mtaani kila akipita mtaani ananyooshewa vidole, akitazama hakuna alichopata zaidi ya aibu anayoendelea kuivuna kila kukicha. Ama kweli mwisho wa ubaya aibu.
Maana tulikuwa tunamwambia mara zote ndugu macho ya mwanadamu hayashibi pia wazuri wapo na wataendelea kuzaliwa je, utawamaliza wote mwenyewe? zaidi tukawa tunamwambia unachofanya ni mbegu utakuja kuvuna yaani unachotenda utatendewa pia. je, utafurahia kuvuna mbegu hii uipandayo? anakinja sura mithili ya kutafuna ndimu anasema kusema ule ukweli sitamani. Kawakatisha masomo mabinti wengi na anawatoto kila mtaa na hawatunzi anajisemea Kwa unyonge na sauti dhoofu isiyosikika vizuri kutoka kitandani pake, "nitakufa kwa majuto makubwa nimefanya mengi maovu, hata sijui sura yangu nitaiweka wapi mbele za muumba wangu.." anaongea maneno haha Kwa uchungu huku yakisindikizwa na machozi yanatiririka mpaka kidevuni.
Tunamwambia tena kila unapopata nafasi ya kuwa hai inamaana unayo nafasi yakutengeza njia yako na kuonyeka pia. Unaweza kutubu na hakika Mungu akakurehemu na kukufutia maovu yako hata akakuponya lakini, usiendelee na uovu uliokuwa ukitenda tubu kumaanisha kuziacha (Mithali 28:13,1Yohana1:9) Lakini ndugu kumbuka katika nafasi hii uliyonayo kuwa Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo shingo yake itavunjika ghafla wala hapati dawa.(Mithali 29:1)
Basi mwishoni tukaomba naye na kumwongoza Sala ya Toba akawa amempokea Yesu. Akawa amepata amaani moyoni na uhakika was maisha take ya Sasa hata baada ya kufa. Na tulimalizia kumwambia kuwa sasa amekuwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya. Tukamsisitiza asijihukumu binafsi na dhamiri yake akumbuke kuwa ameuvua utu was kale, Sasa akazane kusoma Neno la Mungu kuomba, ibada za binafsi na kujumuika na wengine hakika mengi tutazidi kumfundisha.
Imani yangu kuna jambo umejifunza ...
Nakutakia tafakari njema ni mimi ndugu yako nikupendaye sana, Ev. Katana Japhet. usiache kutembelea na kufollow ukurasa wetu Facebook Gospel Stewards Family - GSF uzidi kujifunza zaidi kila siku. pia Subscribe kwenye channel yetu YouTube GOSPEL STEWARDS TV pia huko kuna video nyingi 400+ za Mafundisho.
mawasiliano Zaidi nawe ukitaka kutengeneza njia yako:
©️+255745746691
Ev. Katana Japhet.🇹🇿
Hakuna Raha wala furaha na amani katika kutenda dhambi, jua kabusa ukiendelea kuilea dhambi itakuangamiza hatak**a ni sirini Bora ukajiweka wazi usaidiwe. Tunasema Dhambi inaanza na tamaa, inakomaa kuwa dhambi na mwishowe ni mauti. hero umesikia ujbe huu ni sauti ya Mungu inakuita utubu. ubarikiwe kuitikia wito. usikubali kuendeleaa kuwa mtumwa wa dhambi wakati msaada upo na unaweza kuishi maisha matakatifu.
.
19/11/2025
Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Costa Aba, Daviess Ke Busera, Sikha Mondal, Saimon Mtoto Wa Mungu, Anipha Frank, Martin Shakur, Tonny Mtiaa
14/11/2025
Men Camp is around the corner kindly welcome
13/11/2025
Kwako first year
Karibu darasani
Mafunzo kujiandaa na chuo
+255752352116
Tuna jina lako na chuo chako WhatsApp kujiunga na semina
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Address
Tukuyu
Mbeya
EV.KATANAJAPHET