Mbeya Press Club

Mbeya Press Club

Share

Ukurasa Rasmi Wa Klabu Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Mbeya.

Photos from Mbeya Press Club's post 29/12/2025

MWANDAMBO ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KIJINAI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali ya Saint Clemence, Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni “A” Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashfu imani za dini zingine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga imeeleza kuwa Mwandambo alik**atwa Disemba 29, 2025 majira ya saa nne asubuhi maeneo ya Uzunguni akichapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashfu imani ya dini ya kiislamu na kikristu kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Kamanda Kuzaga amesema upelelezi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

31/08/2025

“Nguvu ya pamoja ni muhimu sana katika kufanikisha ulinzi na usalama wa Waandishi wa Habari” - Wakili Onesmo Olengurumwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), akizungumza katika Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Ulinzi na Usalama wa waandishi wa Habari ulifanyika jiji Dar es Salaam katika Ofisi za UNESCO, leo Agosti 29 2025.

Aidha, Wakili Olengurumwa amemueleza IGP Camilius Wambura ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mdahalo huo kwamba, Jeshi la Polisi linapaswa kuwalinda Waandishi wa Habari kuelekea katika kipinidi cha Uchaguzi huku akiwaasa Waandishi wa Habari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari k**a njia moja wapo ya kukaa katika mstari haki na kujilinda.tanzania

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Sokoine
Mbeya