RhapsodyMan

RhapsodyMan

Share

Influencing the world with the rhapsody of realities, reaching the unreached , touching the untouched.

Mafanikio yenye kuongezeka Daima by Amedeus Live 01/03/2024

Listen to "ror promo 3.mp3" from Amedeus Live on Anchor: https://podcasters.spotify.com/pod/show/amedeuslive/episodes/Mafanikio-yenye-kuongezeka-Daima-e2ggdgr/ror-promo-3-mp3-ab03vsd

Jiunge na chaneli yetu ya Telegram:
https://t.me/amedeuslivepodcast

Mafanikio yenye kuongezeka Daima by Amedeus Live Umeitwa katika umilele. Mungu aweka umilele ndani Yako. Wewe ni k**a mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji. Umeunganishwa na mfumo wa Ugavi wa Mungu.... Mafanikio Yako ni dhahiri, halisi na ya kudumu...

15/02/2024

╔════════════════╗
RHAPSODI YA UHAKIKA
KWA WASOMAJI WA AWALI
╚════════════════╝

👤MCHUNGAJI CHRIS

Alhamisi 15

UNAWEZA KUONA NINI?

Tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele (2 Wakorintho 4:18).

K**a unahisi dalili za homa mwilini mwako, je, mara moja unajiona mwenyewe hospitalini au ukiyakosa masomo shuleni? Au je, unatunza akilini picha ya uponyaji na ukamilifu wako, bila kujali jinsi unavyoweza kuwa na unahisi?

Musa alipotuma watu kumi mbili kwenda kuipeleleza Kanaani, ni Yoshua na Kalebu tu walioona ushindi; wale kumi waliobaki waliweza tu kuona matatizo na kushindwa (Hesabu 14:9). Yoshua na Kalebu walitazama kwa macho ya imani na kuona uwezekano.

Jifunze kuona kwa macho ya imani, licha ya hali inavyoweza kuonekana kuwa ngumu kiasi gani. Kumbuka, “…K**a ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.” (Marko 9:23 NEN). Kwa hiyo, jizoeze mwenyewe kuona uwezekano tu; ona mafanikio, uponyaji, na ushindi.

📖ANDIKO LA KUSOMA
1 Yohana 5:4

🔉SEMA HIVI
Kwa macho ya imani, ninaona uwezekano wa mafanikio, uponyaji, na ushindi. Haleluya!

Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”

Upeleke kwenye kiwango kingine ushiriki wako kwenye Injili kwa kushiriki kwenye ReachOut World Extrvaganza na Mchungaji Chris. Anza sasa hapa bit.ly/RoWLive

Dhamini usambazaji wa Rhapsodi ya Uhakika: Anza leo hapa👉🏾
http://services.tniglobal.org/?center=eastafricacenter4

Jiunge nasi kujifunza Neno la Mungu
WhatsApp:
https://chat.whatsapp.com/FuQEUI0Yg7P0C0mOOkGGd7

Lisikilize Neno la Mungu kwako
Tumeitwa Kutumika https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Tumeitwa-Kutumika-e2e2uld

Vurugu na Hasira-TeeVo
https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kataa-Vurugu-na-Hasira---Rhapsodi-TeeVo-e2e2v0c

Kuangaza Kupitia Roho Mtakatifu
https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kuangaza-Kupitia-Roho-Mtakatifu-e2e537d

Yesu Kristo - Wasifu wa Mungu https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Yesu-Kristo---Wasifu-wa-Mungu-e2e9t01

Uchunge Ulimi Wako https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Uchunge-Ulimi-Wako-e2e9sq7

Lulu nzuri na ya Thamani https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Lulu-nzuri-na-ya-Thamani-e2e9slo

Haki inakufanya Jasiri https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Haki-inakufanya-Jasiri-e2ebl4m

Alibatilisha Mauti https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Alibatilisha-Mauti-e2ef5iq

Hamna Haja Wasiwasi https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Hamna-Haja-Wasiwasi-e2egm8e

Yeye Yuko Juu ya Yote https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Yeye-Yuko-Juu-ya-Yote-e2eqgoo

Kuinuliwa Kwako https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kuinuliwa-Kwako-e2ev7co

Angaza k**a Mwanga https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Angaza-k**a-Mwanga-e2evlf7

Maisha Bora https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Maisha-Bora-e2fa6s3

Kuishi katika Jina lake Lisiloshindwa https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kuishi-katika-Jina-lake-Lisiloshindwa-e2fchh4

Tiketi ya Kupokea kila Baraka https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Tiketi-ya-Kupokea-kila-Baraka-e2ffjbl

Vitu vyote vipi chini ya Miguu yako https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Vitu-vyote-vipi-chini-ya-Miguu-yako-e2fld52

Afya Njema ni Haki Yako. https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Afya-Njema-ni-Haki-Yako-e2flrb3

Mito ya Uponyaji https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Mito-ya-Uponyaji-e2fchco

Tufuatilie
https://amedeuslive.blogspot.com/2024/01/dhamini-teevo-leo.html

Mungu akubariki

account.rhapsodyofrealities.org

17/02/2023

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://rhapsodyofrealities.tniglobal.org

*TUMEUNGANISHWA KWA ROHO NA NENO*

Ijumaa, 17

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*…kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja*_ Yohana 11:51-52

Mistari hapo juu unaleta akilini maneno ya Yesu katika Yohana 10:16. Alisema, _*“Na kondoo wengine ninao, ambao si wa z**i hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja”*_ (Yohana 10:16). Alitoa kauli hii akiwazungumzia Wayahudi na Wamataifa ambao wangelimwamini. Alikuwa anaenda kuwakusanya wote pamoja k**a kundi moja na kuwa mchungaji wao. Ahimidiwe Mungu!

Jinsi gani Bwana Yesu anavyotaka Kanisa liwe wamoja! Anataka tuzungumze kwa sauti moja, tuwe na maono sawa tukijua kuwa tunaye Baba mmoja na Bwana mmoja, Yesu Kristo. Akiwaombea watoto wote wa Mungu kwa Baba, alisema, _*“…ili wawe kitu kimoja k**a nasi tulivyo mmoja”*_ (Yohana 17:22 BHN).

Ndoto ya Mungu ni kuwakusanya watoto Wake katika roho ya umoja. Usilichanganye hili na Dini Moja ya Ulimwengu ambayo wanautandawazi wanajiona bora zaidi wanajaribu kuiunda. Elewa kuwa Mungu anapofanya kitu, Shetani kila wakati anataka kuja na bandia Mungu anatukusanya pamoja, si lazima katika mwili, bali mioyoni mwetu—akituunganisha kwa Roho na Neno.

Leo, wengi wetu, watu wa Mungu duniani, tunafikiri vitu sawa kuhusu Bwana, tunampenda kwa njia ile ile kwa shauku sana, tunaihubiri Injili na kuvuna nafsi kuliko ilivyowahi kutokea. Tunapendana zaidi, na tunaielewa vizuri zaidi, siri ya mwili wa Kristo katika umoja wa roho. Hii ni ndoto ya Mungu, na kila mmoja wetu lazima ajibidiishe kwa ajili ya umoja wa Mwili wa Kristo.

Fikiria kuhusu hilo: kukiwa na wengi wetu tukiwa tunafanya kazi pamoja kutoka duniani kote, tumelifanya Neno la Mungu kupitia Rhapsodi Ya Uhakika lipatikane katika kila lugha iliyo hai duniani. Tumeunganishwa na Roho kwa ajili ya maono sawa na kwa ujumbe mmoja.

Kupitia Roho Mtakatifu, tunaelewa na kutangaza ujumbe mmoja. Hili litaendelea hata kipimo zaidi enzi ya Kanisa inavyokuja mwishoni. Utukufu kwa Mungu!

*| SALA*

*Mpendwa Baba, ninakushukuru kwa ukamilifu na kujengeka kwa mwili wa Kristo. Ahsante kwa uelewa wa kina uliowapa watoto Wako kuuelewa na kuushirikisha ujumbe mmoja, tunavyotimiza ndoto Yako, na kufikia umoja wa imani na wa maarifa ya mwana wa Mungu, hadi kimo cha ukamilifu wa Kristo, katika Jina la Yesu. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** Waefeso 4:13; 1 Wakorintho 12:12-13; Wafilipi 1:27 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Marko 2:23-3:1-12 & Walawi 11-12

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Mathayo 15:10-20 & Mwanzo 48

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye* _*www.rhapsodyofrealities.org*_

15/02/2023

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://rhapsodyofrealities.tniglobal.org

*JENGA KULINGANA NA MAELEZO*

Jumatano, 15

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*…Musa alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano ulioonyeshwa kule mlimani”*_ Waebrania 8:5 NEN

Mungu alipomwambia Musa ajenge hema, Alimpa maelezo dhahiri na kumwagiza ajenge kulingana na maelezo hayo: _*“Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya”*_ (Kutoka 25:9).

Katika mwenendo wako na Bwana na kazi katika Ufalme Wake usikimbie tu na kila wazo kwa sababu hilo ndilo unalodhani ni zuri. Uwe na uhakika kuwa unafuata maelekezo ya Mungu; muundo na maelezo aliyoyatoa. Ni moja ya sababu inakulazimu kulijua Neno wewe binafsi.

Ndani ya Neno Lake utakuta sampuli, miundo na maelezo ya jinsi Anavyotaka tuishi, vitu Anavyotaka tufanye na jinsi ya kuvifanya. Mtunga zaburi alisema katika Zaburi 127:1, _*“BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure…”*_; lazima tujenge sawasawa na mpango Wake.

Katika siku hizi za mwisho, Bwana Yesu analijenga Kanisa Lake. Alisema, _*“…nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”*_ (Mathayo 16:18). Kuna maelezo tuliyopewa ndani ya Neno la Mungu yanayotuonesha jinsi Anavyolifanya hili. Biblia inasema (Kristo Mwenyewe), _*“…aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa”*_ (Waefeso 4:11-12 NEN).

Mpango Wake ni kujenga kupitia viongozi hawa, lakini kila mmoja anahusika, kila mmoja wetu anachangia kwenye ujenzi wa mwili huu mkubwa wa Kristo: _*“Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo”*_ (Waefeso 4:16).

Kila wakati unapomwongoza mtu kwa Kristo unaongeza katika ujenzi wa Mwili wa Kristo, na ni jengo la kifahari sana. Haleluya! Endelea kufanya wajibu wako kwa kuvuna nafsi ziingie kwenye Ufalme. Utakuwa unachangia katika ujenzi huu wa jengo la kifahari sawasawa na maelezo yaliyotolewa.

*| SALA*

*Mpendwa Baba, ninakushukuru kwa uwezo wa Neno Lako rohoni mwangu. Mimi ni mtendaji wa Neno, sio tu msikiaji. Matokeo ya kuishi katika, na kwa Neno yanadhihirika dhahiri katika kila eneo la maisha yangu leo, katika Jina la Yesu. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** Waebrania 8:5 AMPC; 1 Samweli 15:22 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Marko 1:21-45 & Walawi 8

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Mathayo 14:22-33 & Mwanzo 46

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye* _*www.rhapsodyofrealities.org*_

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Chunya District
Mbeya