AFYA BORA
virutubisho na afya ya ngoz
Ugonjwa Wa Kaswende – Syphilis . Ni Nini Chanzo Na Tiba Yake?

Kaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana, mara nyingi kupitia ngono. Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi, au kwenye ngozi laini zenye majimaji za ukeni, kwenye mkundu, na midomo. Kwa hiyo njia kuu ni kupitia ngono ya kawaida, ya kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile. Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara nyingi michubuko hatarishi haitambulikani. Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo kumwambukiza mpenzi wake.
Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia nguo au vyombo vya chakula.
Chanzo Cha Kaswende Ni Nini?
Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum, ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda kwenye midomo au sehemu nyeti.
Mwanamke mwenye mimba na ana ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa. Aina hii ya kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa. Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua – hali inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto wa jicho na kifafa.
Dalili Za Kaswende
Kuna hatua nne za ugonjwa huu wa kaswende. Ni dalili gani utaziona, inategemeanan na ugonjwa upo katika hatua ipi katika hizi nne. Hatua hizi zinaweza kuingiliana na dalili si lazima zitokee kwa mtiririko ule ule. Unaweza pia ikawa na kaswende na usione dalili zo zote kwa miaka kadhaa.
Lakini, hata k**a hujaona dalili zo zote, bado unaweza kumwambukiza mpenzi wako.
Hatua Ya kwanza Ya Kaswende – Primary Syphilis
Dalili za hatua ya kwanza huonekana siku 10 hadi mie
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Morogoro
1255