Health Insurance

Health Insurance

Share

Health Insurance inahusika na utoaji wa Elimu na matibabu ya changamoto mbalimbali za kiafya kwa kutumia Virutubisho Lishe

27/07/2022

Napokea messages nyingi Sanaa kutoka Kwa kina dada kuwa siku hizi kupata mtoto ni Changamoto kwao, lakini hawajui nini Chanzo Cha wao kuwa katika Hali hiyo inayowaletea utata mkubwa Sanaa katika Ndoa zao.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mwanamke, Binti au dada huyo hawezi kubeba ujauzito:
🕳️Kuugua baadhi ya magonjwa ya zinaa yanayopelekea kupata vimbe mbali mbali katika mfumo mzima wa Uzazi k**a vile PID, fibroids na zingnezo
🕳️Kukosa uwiano sawa wa homoni za k**e ni mojawapo ya viashalia vya huyu mwanamke kutokuweza kubeba mimba.
🕳️Kukosa Ute wa Uzazi nyakati za hatari au nyakati ambazo yai limekwisha kupevuka linahitaji kurutubishwa, hii hutokana na baadhi ya njia za uzazi wa mpango k**a sindano vidonge Nk
🕳️Kutokuwa na mzunguko unaoeleweka Kwa mwanamke, hii huchangia asilimia kubwa sanaaa maana Kuna siku maalum TU za mimba kuingia katika mzunguko wa mwanamke kwahy k**a mzunguko haueleweki itapelekea kutoshika mimba
🕳️Kuziba Kwa mirija ya uzazi, hii nayo huchangia dada kutokuweza kutimiza lengo lake la kupakata mtoto inaweza kuwa imevimba au imejaa maji na kupelekea mayai kushindwa kufika sehem ya tumbo Ili kurutubishwa na mbegu za kiume
🕳️Wengine chango la uzazi hupelekea wasipate mimba, pamoja na adha nyinginezo chango hufanya mimba kutokutungika
🕳️Zipo sababu zingine k**a vile kutoa mimba mara Kwa mara, kuwa na Msongo wa mawazo, uzito kuwa mkubwa sanaaa nayo ni sababu inachangia kukosa mtoto.

Kwa ushauri, maoni na maswali wasiliana nasi Whatsapp no 0710705676
Health Insurance
Office zipo:Moro, dar, Dodoma na Mbeya

01/11/2021

FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST )

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (o***y) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana k**a ovarian cyst.
Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.

MAYAI YA MWANAMKE
Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus).
Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana k**a o**m ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (o***y) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.
Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila ovari na hii ndio hujulikana k**a ovulation au upevukaji mayai. Mayai haya ya uzazi huishi kwa saa chache hadi saa 24 ikiwa hayatorutubishwa na mbegu za kiume.
Mabaki ya mfuko wa mayai ya uzazi yanayojulikana k**a follicle ndani ya ovari, hugeuka na kuwa corpus luteum ambao huhusika na utoaji wa kichocheo au homoni aina ya progesterone kwa wingi.
Homoni hii ya progesterone ndio inayosababisha mfuko wa uzazi kujiandaa kwa kujikita yai (implantation) lililorutubishwa kwa mbegu ya kiume ndani ya mfuko wa uzazi kwa kuongeza unene kwenye kuta zake. Yai hili husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ambako hukua na kuwa mtoto. K**a upachikwaji wa yai liliorutubishwa hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, corpus luteum huanza kusinyaa na kupotea na kusababisha kushuka kwa kiwango cha homoni aina ya progesterone na estrogen.
Kushuka kwa kiwango cha vichocheo hivi ndio husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai la uzazi na ndipo pale mwanamke anapoanza kuona siku zake za hedhi(kutokwa na damu ukeni).

UVIMBE KWENYE MAYAI.
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke ila aina hizi saba ndio huonekana sana kwa wanawake wengi.

1~ Aina ya kwanza ni Follicular cyst ambayo uvimbe hutokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi.
Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya ovulation.
Kwa kawaida uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.

2~Aina ya pili ni Corpus Luteum cyst- ambao ni uvimbe unaosababishwa na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida corpus luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwengine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe.
Uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.

3~Uvimbe wa tatu ni Hemorrhagic cyst- Uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke.

4~Uvimbe mwingine ni Dermoid cyst- ambao sio saratani na pia hujulikana k**a mature cystic teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na cartilage.
Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.

5~Aina nyingine ni Polycysitic appearing cyst- ambao unakuwa mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

6~Aina ya sita ya uvimbe ni Cystedenoma-Ni aina ya uvimbe unaotokana kwenye tishu za ovari na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.
7~Aina ya mwisho ya uvimbe unaowapata wanawake ni Endometriomas /Endometrial.

SABABU ZA UVIMBE.
Vihatarishi vya tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke nipamoja na
historia ya awali ya ovarian cyst. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa nao wakapatwa na tatizo hilo.
Sababu nyingine inayoweza kusababisha uvimbe katika mayai ya mwanamke ni kuwa na mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum. Kihatarishi kingine ni kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili na hii ni kwa wale wanawake wanene.
Ugumba na kuvunja ungo mapema ni sababu nyingine ambapo mtoto wa k**e hasa anayevunja ungo akiwa na miaka 11 au chini ya hapo huweza kupatwa na uvimbe katika mayai yake.

DALILI;
Maumivu makali, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, ambapo maumivu hayo yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja.
Kuhisi tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba, maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum, maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati wa hedhi na ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya chini mgongoni. Maumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya kukutana kimwili, kuhisi kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni. Dalili nyingine ni ugumba na kuhisi uchovu, mabadiliko ya haja ndogo yaani kukojoa mara kwa mara, kujikojolea au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo.

VIPIMO
Mgonjwa kufanyiwa Endova**nal Ultrasound ambayo hufanywa kwa kuingiza mpira maalum kupitia ukeni na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua k**a uvimbe kwenye mayai ni wa aina gani na kujua k**a ni maji tu (fluid filled sac), au ni maji pamoja na mchanganyiko wa vitu vigumu kwa maana ya complex, au ni vitu vigumu pekee ambapo huitwa completely solid

Kumbuka uvimbe huu sio kansa hivyo ondoa hofu. Mbali na donazole ambayo ni ya gharama na haishauliwi itumiwe kwa mda mrefu ina sababisha mwanamke anakua na sifa za kiume.UKIFANYIWA OPERATION USIDHANI UVIMBE UMEISHA UNAOTA PEMBENI HADI UTAKAPOWEKA VICHOCHEO SAWA.
Sasa suluhisho lako lipo tuna dawa ambao imetengenezwa kitalamu katika mfumo wa vidonge na vimetengenezwa kwa mimea baada ya utafiti na majaribio ya kutosha na viwanda vya madawa vikubwa hapa duniani.
Utapata suluhisho lako bila madhara kwani ni mimea 100%.
Hii dawa inapunguza uvimbe wa fibroid bila madhara k**a donazol. K**a una ndugu au rafiki mwambie suluhisho lipo na mshirikishe kuokoa afya yake.
Kwa maoni na ushauri na tiba tuandikie kwa namba
0710705676

18/10/2021

*NINI CHANZO CHA UKE KUWA MKAVU?*

Uke mkavu; ni tatizo ambalo husababishwa na upungufu wa homoni au kutokua na uwiano wa homoni ya estrogen ambayo hupelekea misuli ya uke kusinyaa na kukosa *vilainishi.*

Kwa kawaida uke unatakiwa kuwa na Ute wa wastani ambao hufanya uke kubana kuleta joto na Raha ya tendo.
Ute huo ukizidi Sana au kua pungufu Sana nalo ni tatizo.

*VISABABISHI VYA UKE MKAVU.*
👉🏿Utumiaji mafuta yenye kemikali (cosmetics)
👉🏿Magonjwa ya zinaa na fangasi.
👉🏿Matumizi ya sabuni za antibiotics kwa kuoshea uke.
👉🏿Upungufu wa homoni.
👉🏿Uoga na wasiwasi

*DALILI ZA UKE MKAVU*
👉🏿Maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉🏿Kupungua hamu ya tendo la ndoa
👉🏿Kua na ngozi kavu
👉🏿Maumivu ya mifupa na viungo
👉🏿Msongo wa mawazo
👉🏿Mzunguko wa hedhi Kubadilika badilika
👉🏿Kutokufurahia tendo la ndoa kutokana na Maumivu.
*MATIBABU YA UKE MKAVU*
Kuna lishe ambazo zimetengenezwa kwa kuzingatia tiba lishe na Ni Bora Zaidi kwa afya

0710705676
WhatsApp na sms za kawaida

Want your business to be the top-listed Finance Company in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address


Kihonda
Morogoro