Dondoo ZA AFYA

Dondoo ZA AFYA

Share

Health and Wellness

05/09/2024

*MVURUGIKO WA HOMONI (HORMONAL IMBALANCE)*

Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa vichochezi katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo kufanya mwili kubadilika. Mvurugiko wa homoni kwa mwanamke huweza kuchangiwa kutokuwepo na usawa katika homoni za Estrogen na progesterone. Kupungua au kuzidi kwa homoni hizi hupelekea mvurugiko wa homoni kwa mwanamke.

*VYANZO/SABABU ZA MVURUGIKO WA HOMONI*

✓Uwepo wa sumu mwilini hasa katika ✓mfumo wa damu.
mfumo mbovu wa maisha. Hili ni janga kwa magonjwa mengi yasiyoambukizwa kwasababu watu wengi wameondokana na vyakula vya asilia.
✓Umri ukienda sana hasa wakati mwanamke akifikia kipindi chaKukoma kwa hedhi miaka 45+
✓Kutofanya mazoezi, na kutokulala masaa anayostahili kwa siku kwa sababu watu wengi tuko bize kupita kiasi ✓Uzito mkubwa kwa mwamke
✓Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa huwa pia inaweza kuathiri mfumo wa hedhi.
✓Msongo wa mawazo. Hili ndilo janga linaloongoza kwa kuvuruga hormoni kwa kuwa wanawake wengi siku hizi wanaishi kwa Msongo mkubwa.
✓Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango k**a vidonge,sindano na njiti.
✓Utoaji wa mimba. Dada zangu hii inawahusu ni chanzo kikubwa cha Mvurugiko wa homoni ikijumuisha mzunguko wa hedhi.
✓Historia ya familia(Upungufu au ongezeko ya homoni ya progesterone na Estrogen)

*DALILI ZA MVURUGIKO WA HOMONI*
>Ukavu ukeni
> >Maumivu wakati wa tendo la ndoa
>Kutoa jasho usiku
>Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi
>Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa
>Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku 7. (heavy bleeding, au kujaza pedi moja kwa saa moja)
>Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi
>Uchovu wa mara kwa mara
>Hasira za mara kwa mara
>Kukosa usingizi
>Homa za usiku na Kizunguzungu cha mara kwa mara
>Mzio wa vyakula (Allergie), kuchagua chagua vyakula
>Ongezeko ya tumbo na nyama uzembe
>Kuharibika kwa ngozi (chunusi, vipele… n.k)
>Maumivu ya viungo
>Kupata hedhi wakati wa ujauzito (progesterone ikiwa imezidi)
>Kutokupata hedhi (balehe) adi umri wa miaka 20 na kuendelea
>Mwili kutokukua, kuonekana k**a binti mdogo, na kutokukua kwa via vya uzazi
>Kusinyaa na kupauka kwa ngozi wakati wa siku za hedhi na wakati wa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango
>Maumivu ya kichwa mara kwa mara
>Kuwa na tabia ya hamaki (kukosa utulivu)
>Kutokupata choo kwa wakati
>Misuli kudondoka

*MADHARA YA MVURUGIKO WA HOMONI*

Pamoja na dalili nyingi tulizoziona wanawake wanapaswa waelewe vitu vifuatavyo hutokea ;

_Ukiendelea kubaki na dalili tajwa hapo awali kwa muda mrefu, kinga ya mwili itashuka kwa kiasi kikubwa na kusababisha madhara mengi k**a yafuatayo:

_Kutoshika ujauzito kwa muda mrefu
_Mimba kuharibika mara kwa mara
_Kukosa mtoto au Ugumba
_Maumivu wakati wa tendo la ndoa
_Kuwa na tabia na maumbile ya kiume
_UTI (Urinary Tract Infection) ya mara kwa mara
_Kuzeeka mapema
_Kuziba kwa mirija ya uzazi
_Saratani ya shingo ya KIZAZI
-Uvimbe kwenye uzazi wa mwanamke (Fibroids and Cysts)

*Kwa ushauri na tiba wasiliana nasi
0716161433 / 0710727648

Want your practice to be the top-listed Clinic in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Morogoro