Professor Jay

Professor Jay

Share

MIKUMI Stand UP�

19/04/2026

Dada mkuu KASHASEMA❤️❤️❤️❤️

"1st May

Ombi langu kuu ni mjitokeze kwa wingi sana kushuhudia ukuu wa Mungu.

17/04/2026

"PROF JAY NI GIANT GORILLA WA BONGO FLAVA

KUTAMBULISHA albamu ya Machozi, Jasho na Damu, ilitoka "Bongo Dar es Salaam", "Jina Langu", halafu "Ndiyo Mzee". Mikwaju mingine iliyofuata ni “Piga Makofi” aliowashirikisha Simple X na Sos B, “Niamini”, aliofanya na familia yake ya HBC, Big W***y na Fanani. “Tathmini” alibatua na Jay Moe, “Nawakilisha”, aliowaalika AY, Black Rhino, Complex na Adili.

Vyuma vingine ni “Na Bado”, “Salamu Bibi na Babu”, “Yataka Moyo” na “Machozi, Jasho na Damu”, uliobeba jina la albamu. Fanya mapitio upya kuanzia mwanzo. Hesabu ni tracks 11. Urefu ni dakika 53. Ukianza kusikiliza, hakuna kupeleka mbele wala kuskip, kila tufe lina-makes sense. Hii ndiyo mantiki huwa hakuna ubishi, Machozi, Jasho na Damu inapotajwa kuwa ni moja ya albamu bora kabisa za Bongo Flava.

Albamu mbili; Funga Kazi 2000, vilevile Machozi, Jasho na Damu, zilitosha kumpa Prof Jay legendary status si tu kwenye jumuiya ya Hip Hop Afrika Mashariki, bali kwa sanaa ya Afrika. Jay ni legend. Jay ni giant gorilla. Vyovyote unavyoweza kumtafsiri, Jay ni monstrous size kwenye utamaduni wa Bongo Flava.

Machozi, Jasho na Damu ilitoka Desemba 2001. Mwaka 2002, yalikuwa majuma 52 ya makusanyo kwa Prof Jay. Show mkoa kwa mkoa, hadi kuvuka mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati huohuo ilikuwa miezi 12 ya hekaheka za jikoni, maandalizi ya pishi jipya, Bongo Records, kwa audio engineer, P Funk Majani.

“Priii priii eti promota anabeep, naamua kumpigia bila aibu anajisifu,” ilikuwa salamu ya Prof Jay, jina la wimbo ni “Promota Anabeep”, with Mgosi Mkoloni, michambo mikavu kwa Nyangema Promota aliyevaa suti na kandambili. Anamwahidi msanii paradiso, halafu anampiga kizinga cha nauli na kugongea fegi. “Nyambaaf”, kwa sauti ya Mkoloni. Ndivyo albamu “Mapinduzi Halisi”, ilivyotambulishwa.

Desturi ya Jay ilikuwa kuandika historia katika kila albamu, ndivyo alivyofanya kwenye “Zali la Mentali” ndani ya Mapinduzi Halisi.

Unaweza kuzuia mvua lakini siyo heshima ya Prof Jay kwenye Bongo Flava. Mei Mosi, 2026, Bongo Flava Honors itafanikisha the long overdue induction ceremony ya Jay. 710 Garden, Kawe historia itaandikwa. Sugu The Jongwe atasherehesha tukio.

Ndimi Luqman MALOTO".

08/04/2026

"Big vibes. Bigger energy. 🔥✨

Deiwaka World Bongo Flava Honors – Season 4 is here! 🇹🇿🎶
A night to celebrate the culture, the sound, and the stars shaping Bongo Flava.

🎤 With Prof Jay
🎙 Hosted by Sugu
📅 May 01 | 8PM – 12AM

🎟 Grab your tickets now on the Tukiio App & website

".

01/04/2026

"CHEMSHA BONGO YA JAY ILILETA MAPINDUNDUZI YA UTAMADUNI

N***A Jay, msongo ambaye maskani kwake ni Kimara, alibaini mapema kuwa mwarobaini wa wapinga Swahili Rap ni maudhui ambayo wasingeweza kuyapinga. Kutoka Kimara mpaka Upanga, ndani ya familia kubwa ya Hard Blasterz Crew (HBC), The Scientist Prof Ludigo Bishota, alinyonga midundo, Jay akawa tonic kwenye albamu ya Funga Kazi 2000.

Ngoja kwanza, kabla ya kudurusu albamu, tuzungumze kuhusu Chemsha Bongo. Wimbo ni baraka kwa kila sikio. Ulikuwa chachandu kwa vipindi vyote vya redio. Uliongeza idadi ya wasikilizaji wa redio, ukakuza namba ya wafuasi wa Swahili Rap. Ukawapa wazimu vijana wengi, wakatamani kufanya muziki wawe k**a N***a Jay. Hili halibishiwi, Chemsha Bongo ilizalisha underground wengi wa Rap Afrika Mashariki.

Wazee wakaksi walinywea, wakatoa leseni kwa watoto wao waliorap. Wazazi wengine waliwauliza vijana, “wewe hufokifoki, hutaki kuwa k**a yule wa Chemsha Bongo?” Mabitozi kibao wakajiita “Jay Tunakuzimia”, na walifanikisha mitikasi ya pesa na kuchezea nyoyo za warembo waliompenda N***a Jay. Ilikuwa analogia. Anasikika redioni, picha yake haijulikani. Matapeli wali-take advantage.

Chemsha Bongo ilikuwa lead single ya Funga Kazi 2000, ingawa release namba moja ilikuwa “Chuzi Limekubali”. Halafu sasa, ikafuata “Mamsap”. Wahuni walilia mapenzi kwa unyenyekevu na uadilifu mkubwa. Jay alikamua beti mbili, romantic gangsta mwenzake, Terry Fanani, akaua moja ya kati. Mamsap ni kibali kwa gangstaz kunyenyekea na kulia mapenzi pindi nyoyo zinapok**atika.

Tazama akili ya Jay; watu wanasema Rap uhuni, yeye akatumia maarifa yake makubwa ya kusimulia, akatoa hadithi ya mwanampotevu kutoka familia ya kitajiri, aliyekataa shule, akaishi pepo ya mpito kwa sababu alikuwa na fedha. Ponda sana raha, hakusikia la mwadhini wala la mnadi sala. Mwisho, kijana anajuta na kutubu baada ya kufilisika. Je, nani angeweza kupingana na ujumbe huo wenye mafunzo? Chemsha Bongo ika-dominate.

Elewa tunaposema Jay ni foundational lifter wa Bongo Flava. Mei Mosi, 2026, 710 Garden, Kawe, Jay atasimikwa rasmi heshima ya Bongo Flava Honors. Madude ya Jay yatalia kwa live band. Sugu the Jongwe atakuwa mwenyeji.

Ndimi Luqman MALOTO".

11/08/2025

MASKANI KIMARA watu kila siku Mamtoni,
Jonas Kiwia wasalimie Washington,
Ukiweza Pita Texas Mpe HI Chief SAM na mkumbushe uzushi wa BONGO DAR ES SALAAM💣💣💣🔥

Proff Jay x Jose Chamillion Feat. Q Chief - Ebenezer (Official Video) 20/06/2025

https://youtu.be/t29gZ9IFA10?si=p7wXwTsI6RCjG6Gi

Proff Jay x Jose Chamillion Feat. Q Chief - Ebenezer (Official Video) Music Video by Professor Jay featuring, Jose Chameleone Featured Q Chief performing "EBENEZER" (Official Release 2025), The music Video was shot in Dar es Sa...

Want your establishment to be the top-listed Arts & Entertainment in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Morogoro