SEPRO
Ni mpango wa kuelimisha vijana ili kuweza kujitambua katika kufanya mambo mbalimbali ya kijamii,kiuc
31/08/2024
*Mzazi unakumbuka utotoni mwako wakati anakwenda shuleni uliambiwa nini* ?
Mtoto anayesoma hutegemea vyanzo vitatu vya malezi. Ambavyo ni
👉mzazi
👉walimu na
👉jamii inayomzunguka.
Katika malezi hayo yote, malezi ya wazazi huwa na nguvu kubwa kwa mtoto ulikinganisha na vyanzo vingine vyote. Maisha ya wazazi yanachangia mtoto kukua katika njia iliyonjema au mbaya.
Watoto hupenda sana kuwaiga wazazi kwa sababu huwa wanaamini kuwa mzazi ndiyo Mwalimu sahihi. Kwa hiyo kwa njia yote ile mtoto hutafuta kuwafanana wazazi wake. Hapa ndipo methali isemayo, samaki mkunje angali mbichi, mtoto wa nyoka ni nyoka, mama ni Mama hata k**a ni rikwama nk. Hutufundisha.
Mzazi anatakiwa kumlea mtoto katika malezi ya kiutu, kielimu, na kiroho.
Tukianza na elimu, mzazi anawajibu wa kufanya kila linalowezekana ili kumsaidia mtoto aweze kufanikiwa katika ndoto ya elimu. Ufuatao ni ushauri wa kumsaidia mtoto ili afaulu mtihani:
👉Mzazi mwambie mwanao, furahia kusoma na penda kujisomea Kwa bidii
👉Lengo la kwanza la elimu ni kumkomboa mtu kifikira, ndiyo maana tunasikia elimu ni ukombozi.
Itashangaza pale ambapo mtu msomi anafanya vitu ambavyo kwa jamii ni chini ya kiwango; wizi, uasherati, madawa ya kulevya nk.
👉Wasomi ni wengi lakini ajira ni chache, hakikisha usomi wako haujitenganishi na shughuli za kila siku za jamii mfano kilimo, ufugaji, biashara, nk.
👉Ingia darasani na sikiliza kwa makini anachofundisha Mwalimu
👉 Hakikisha unaandika alichofundisha Mwalimu kwa mwandiko mzuri
👉Kuwa na ratiba ya kusoma nje ya ratiba ya shule inayotumiwa na walimu kufundishia
👉Baada ya masomo, jikumbushe mlichosoma kwa njia ya kukiandika katika mhitasari
👉baada ya kusoma penda kuwashirikisha wenzako ulichoelewa
👉Kuwa na vikundi vya kujisomea ( group discussion)
👉Jenga urafiki na walimu, usiogope kuuliza ambapo hujaelewa
👉Penda kwenda maktaba kujisomea vitabu
👉 Jiamini kuwa unaweza fanya vizuri, usikubali kukata tamaa
👉rudiarudia mlichosoma darasani
👉k**a mwanafunzi waza masomo
👉Usiwe chanzo cha makundi maovu au kujiunga na makundi maovu
👉 Epuka maisha ya kujitenga na wenzako
👉 Kumbuka kutunza afya, fanya mazoezi, kula, kunywa na maji nk.
👉Kuwa na mahusiano mema na wanafunzi wenzako
👉Usipende kuhairisha mambo k**a kutofanya mazoezi ya darasani na kazi wanazotoa walimu darasani
👉Heshimu na ishi karidi ya sheria na taratibu za shule
👉Tambua vipaji vyako na uvitumie
👉 Kumbuka kusali/ kumtanguliza Mungu katika masomo yako.
👉Acha kuchagua masomo kutokana na sababu zisizo za maana
Mengine k**a mzazi jisemee kadiri unavyomfahamu mtoto wako.
ujana waleo ni uzee wakosho.
..
03/08/2022
WEKA NAFASI NDANI YAMOYO WAKO
Chuki unayoijenga ndani yamoyo wako juu yamtu hakikisha unaipa nafasi kwani ipo siku utahitaji uwepo wa unayemchukia hapo ndipo utajenga mapigano yanafsi.Binadamu tumeumbiwa kukosea,kusamehe nakusahau ukitambua hivi upendo utaupa nafasi,chuki utazipa nafasi na hasira pia utazipa nafasi kwakutambua uthamani wamtu hauna ukomo ukiukosa leo si kwamba hautauhitaji milele.
05/06/2022
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Morogoro