New_Drop_News

New_Drop_News

Share

This is the page of social, economic, political and sports news.

14/07/2023
13/07/2021

Naitwa sanze nna miaka 14,ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wawili,Mdogo wangu anaitwa Simoe ana miaka 11.Ni watoto wapekee katika familia ya Mzee samson.

Baba yetu ni fundi ujenzi,Mzee ambaye anajitahidi kutafuta pesa ili zikaishie kwenye ulevi,Baba ambaye hatujali kwa chakula wala mavazi.Nguvu kubwa ya malezi yetu ilikuwa inatoka kwa Mama,
Mama ambaye ni mlemavu wa mguu na alitumia muda mwingi kukaa chini kwa ajiri ya kuponda kokoto ili tuweze kujipatia kipato kwaajiri ya kukidhi mahitaji madogo madogo.

Mama alilazimika kujiongeza katika utafutaji na akabuni biashara ya mboga mboga za majani,Biashara ambayo mimi na mdogo wangu Tuliitembeza mtaa kwa mtaa uku tukiwa tumeibeba katika mabeseni kwaajiri ya kutafuta wateja.
Safari ya maisha yetu ilikua ni ngumu sana hasa ukizingatia umri wetu ulikua ni mdogo sana ,Tulipaswa kuwa shuleni ila shida zimelazimisha tuwe mtaani na Watu wanao tuzunguka wametupa jina (Chokolaa).
Maisha yalizidi kusonga mbele Mama hakujali ulemavu wake alizidi kupambana kwaajiri yetu na kauli yake kubwa aliyokua akituambia ni kuwa '"siku moja tutasoma" ,Kauli hii ilitupa sana Imani lakini siku zilikua zinazidi kwenda ,Umri unazidi kwenda na kauli ya mama haitimii.

Siku moja baba aliludishwa nyumbani akiwa amebebwa na watu walio dai kuwa wamemuokota njiani huku akitwokwa na mapovu mdomoni..........

Itaendeleaaaaaa

Want your business to be the top-listed Media Company in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Mafisa
Morogoro