Ujenzi on Point

Ujenzi on Point

Share

Pata Huduma ya Ramani na ushauri kuhusu ujenzi

Photos from Ujenzi on Point's post 20/04/2024

Miliki nyumba yako kwa kuanza ujenzi na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana.Hii inafaa sana kwa wanaoanza maisha, Ramani ina vitu vifuatavyo:-
~vyumba viwili vya kulala vyote vya kawaida
~sebule
~jiko
~public toilet na Bafu la kushea
~Baraza Moja { Entrance veranda}
~Ukubwa wa Ramani ni mita 7.5 urefu kwa mita 7.9 upana.
~Mahitaji: Tofali 1400 {za block kuanzia msingi mpaka boma}, Bati 38 { za urefu futi 10 na upana futi 3}. Kupata Ramani hii na nyingine Kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇 https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Photos from Ujenzi on Point's post 13/04/2024

Jenga kwa Ramani kwa sababu nyumba ni Ramani.Jipatie Ramani hii ya vyumba vitatu, chumba kimoja masta, vyumba vingine viwili ni vya kawaida, pia ina;
~Sebule
~dining{chumba cha kulia chakula}
~Jiko
~Choo cha kushea na Bafu
~Baraza ya mbele na ya jikoni { Entrance & Kitchen Verandah}

~Ukubwa wa Ramani ni mita 11 urefu kwa mita 12.8 upana
~Mahitaji: Tofali 3000 { Tofali 1000 za msingi na Tofali 2000 za Boma} Bati pisi 70 { Bati za futi 10 urefu na upana futi 3}
~Kupata Ramani hii pamoja na nyengine kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Photos from Ujenzi on Point's post 13/04/2024

UMUHIMU WA KUJENGA MSINGI IMARA KWENYE NYUMBA YAKO:

Moja ya maamuzi mabovu kabisa ambayo hutakiwi kuyafanya linapokuja swala la ujenzi wa nyumba yako ni kutokujenga msingi imara.

Leo rafiki yangu napenda kukushirikisha umuhimu wa kuwa na msingi imara. Utaweza kufahamu msingi imara ni upi na ni kwa namna gani utahakikisha unakuwa na msingi imara kabisa ili ujihakikishie ujenzi wa nyumba bora.

Msingi Imara kwa ufupi ni ule ambao unaweza kuhimili uzito wa jengo pamoja na nguvu kutoka nje k**a vile upepo, msukumo wa udongo, mitikisiko pamoja na nguvu nyingine za asili. Msingi huu unaweza ukajengwa kwa kutumia mawe, matofali ya block, Zege au malighafi nyingine ambazo zinakubalika kwenye ujenzi. Unapokuwa na msingi imara unajihakikishia usalama wako, mali zako na wote watakaoishi ndani ya nyumba yako na pia utaweza kujikinga kwa namna Fulani na majanga ya asili k**a vile matetemeko na mitikisiko ya ardhi.

Hatua Tatu Muhimu Ujenzi wa Msingi Imara:

~Namna ya kuhakikisha unajenga msingi imara
Ili kuweza kujenga msingi imara na utakaosaidia kuimarisha jengo lako zingatia mambo yafuatayo;
i. Fanya utafiti wa eneo lako hasa katika kutambua aina ya udongo
Hapa unaweza ukafanya hata utafiti wa macho tu na kwa kushirikiana na mtaalamu wako wa ujenzi ukaweza kufanya maamuzi ya msingi utakaohitajika. Wakati mwingine udongo wa juu ya ardhi unaweza ukawa tofauti na ule uliopo ndani ya ardhi baada ya kuchimba mita kadhaa na endapo utakutana na hali hii basi msingi wako itabidi ubadilike kulingana na aina ya udongo uliyokutana nayo. Cha kuzingatia hapa ni kuhakikisha msingi wako unakaa juu ya sehemu ngumu na imara ili kuepuka kutitia.

ii. Tambua k**a eneo lako lina maji maji au ni eneo kavu
Msingi unaojengwa sehemu zenye majimaji ni tofauti kabisa na msingi utakaojengwa sehemu kavu. Kwa eneo ambalo lina maji muda mrefu msingi wake utahitaji material (mali ghafi) zinazoweza kuhimili uwepo wa maji k**a vile zege. Ukijenga msingi wa matofali ya kawaida kwenye eneo hili unajiweka kwenye hatari kubwa sana

iii. Jua matumizi sahihi ya Jengo lako
Kwa kutambua matumizi sahihi ya jengo lako kunasaidia sana katika kutambua uzito sahihi utakaohitajika kubebwa na msingi wako. Msingi wa nyumba ya kuishi ni tofauti sana na msingi wa ghala hivyo usijenge nyumba ya kuishi halafu baada ya muda unaibadilisha na kuwa ghala utaleta matatizo kwenye msingi.

Ninachotaka kukukumbusha rafiki yangu leo ni kwamba msingi ndio sehemu ya kwanza muhimu kwenye jengo lako na kamwe hutakiwi kufanya makosa kwenye eneo hili.

Kitu kingine ambacho ningependa kusisitiza ni kwamba USIJENGE KWA MAZOEA. Epuka kabisa maneno ya mtaani eti mbona Fulani amejenga hivi au vile na wewe ukayapokea yalivyo. Itakapotokea tatizo itakuwa ni wewe na wale watakaokuwa wanaishi ndani ya nyumba hiyo.

Jenga msingi imara uwe na nyumba bora maisha yako yote. Kwa mahitaji ya Ramani mbalimbali na ushauri kuhusu ujenzi Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Photos from Ujenzi on Point's post 12/04/2024

Ramani ya nyumba ndogo yenye mahitaji muhimu, ina..
~Sebule
~dining
~vyumba viwili vya kulala kimoja master
~jiko
~public toilet
~entrance veranda {Baraza ya mbele}
~kitchen veranda { Baraza ya nyuma}
RAMANI INA UKUBWA WA MITA 8.8 UREFU KWA MITA 10 UPANA
MAHITAJI:
TOFALI 1800 ZA BLOCK (Kuanzia msingi mpaka Boma)
BATI PISI 45 (za futi 10 urefu na upana futi 3) Kupata Ramani hii na nyingine kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza Link hapo chini 👇 https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Photos from Ujenzi on Point's post 12/04/2024

Nyumba ni Ramani, Anza ujenzi wako na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana ( Simple Design) Haina mambo mengi.Ramani ina vitu vifuatavyo:-
~Vyumba vitatu vya kulala kimoja ni master
~choo cha public
~Jiko
~Sebule
~Baraza ya nyuma na mbele {Entrance & Kitchen verandah}
~Mahitaji:
Matofali 2000 ya block ya kuchoma ni 4000
Bati 60 za futi 10 urefu na upana futi 3

Ramani ina ukubwa wa mita 10.4 urefu na upana mita 10.3
Kupata Ramani hii na nyingine Kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au bonyeza link hapo chini 👇
https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Want your business to be the top-listed Contractor in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Moshi