Cetosude

Cetosude

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Cetosude, Nonprofit Organization, Sabasaba Soweto, Moshi.

Photos from Cetosude's post 25/09/2025

✨ Fursa Plus Project ✨

Fursa Plus Project ni mpango unaoendeshwa na vijana wenye utaalamu wa kilimo, ufugaji na ujasiriamali, chini ya CETOSUDE.
Lengo kuu ni kutoa elimu ya kilimo-biashara, ufugaji wa kisasa na ujasiriamali wa vitendo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na utegemezi wa ajira pekee.

🎯 Malengo ya Fursa Plus Project

βœ… Kuelimisha vijana na jamii kuhusu kilimo na ufugaji wa kisasa wenye tija
βœ… Kuwafundisha mbinu za kugeuza kilimo na ufugaji kuwa biashara
βœ… Kuwezesha watu kuunganishwa na masoko ya uhakika
βœ… Kufungua milango ya fursa mbalimbali za kiuchumi
βœ… Kuinua kipato na kupunguza umasikini kupitia elimu ya vitendo na darasani

πŸ’‘ Kwa nini Fursa Plus?
🌿 Tunatoa maarifa ya vitendo (practical skills) ya kilimo na ufugaji yanayoweza kutumika mara moja shambani, bandani na sokoni
🌿 Tunawaunganisha vijana na wadau wa kilimo, ufugaji, masoko na fursa za kifedha
🌿 Tunajenga jamii inayojitegemea, badala ya kutegemea ajira pekee

🌱 Kauli Mbiu Yetu:
β€œKilimo na Ufugaji wa Kibiashara, Ujasiriamali wa Vitendo – Fursa kwa Kila Mtu!”

πŸ‘‰ Karibu ujifunze, ushiriki na ufaidike na Fursa Plus Project.

πŸ”— Tembelea: www.cetosude.or.tz

πŸ“© Wasiliana Nasi Moja kwa Moja kwa Taarifa Zaidi:
πŸ“ž Simu: 0621114769/0684772756
πŸ“§ Barua pepe: [email protected]

Photos from Cetosude's post 19/08/2025

Leo tumekamilisha kuunda Team ya wataalamu vijana ambao wataenda kuwatembelea wafugaji katika wilaya ya HAI -Hasa kwasasa tukilenga kata Tatu za mradi ambazo ni machame uroki,machame kaskazini na masama kusini.

Wataalamu hawa watafanya kazi hii mpaka Tare 30 mwezi wa nane tukiwa na lengo la kupitia kila Mfugaji na ikiwa na idadi ya wafugaji 480 +.

From Aid to Trade-FA2T. Project

Facebook Tanzania Women Research Foundation - Tawref Wizara ya Kilimo

Photos from Cetosude's post 14/08/2025

Tumeweza kufanya kikao cha mwongozo na Team ya wataalamu watakayo enda field. Zoezi hili ahirikishi liliongozwa na Team ya CETOSUDE sambamba na viongozi wa kata tatu za mradi.

Huu nimwendelezo wa ushirikiahaji wa jamii yote kuleta mabadiliko hasa kimamuzi.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Sabasaba Soweto
Moshi