FAPRO NGO's

FAPRO NGO's

Share

TO GIVE THE KNOWLEDGE ABOUT AGRICULTURE PODUCTION AND MANAGEMENT PRACTISES

05/05/2022

viwavi jeshi vamizi(fallarmyworm)

Viwavi jeshi vamizi ni wadudu waharibifu ambao walianza kuonekana Afrika Mashariki kuanzia mwaka 2016.Wanaweza kuwa na rangi nyeusi, kahawia au kijani

Wanakula mimea zaidi ya aina 80.Wanaharibu zaidi mimea jamii ya nafaka ingawa mazao hayo yakiwa hayapo wanaharibu sana pamba.

Asili na Usambaaji wa Kiwavi jeshi vamizi (Fall Armyworm)

Asili yake ni Amerika ya kati na kusini a -Machi, 2017Mwaka 2016 alionekana nchini NIGERIAZaidi ya nchi 20 za Afrika zimevamiwa na mdudu huyuTanzania alionekana katika mikoa ya Ruvuma,Rukwa na mbeya mwaka 2017Zaidi ya mikoa 20 TZ imeshavamiwa na FAW-Machi, 2018

MZUNGUKO WA MAISHA YA KIWAVI JESHI VAMIZI (FALLARMYWORM



TABIA ZA NONDO WA KIWAVI JESHI VAMIZI

Huonekana kwa urahisi nyakati za usikuAna uwezo wa kuruka umbali kilometa 100 kwa usiku mmojaAnataga mayai 50-200 kwa mafungu Mayai hufunikwa na utando mweupe Mayai huanguliwa kati ya siku 2 hadi 5 kuwa funza Funza hutapakaa kwenye majani na huanza kula majani upande wa chini ya mmea Funza ni waharibifu zaidi muda wa asubuhi sana na jioni Funza hutoa kinyesi kinachomkinga asiliwe na wadudu wengine au sumu isiweze kumfikia

NJIA ZA KUDHIBITI NONDO NA FUNZA WA KIWAVI JESHI VAMIZI

Kagua shamba lako mara kwa mara ili uweze kutambua k**a nondo, mayai, funza au viashiria au dalili za uharibifu katika zao la mahindi na mimea ya nafaka au mipamba na uchukue hatua zinazostahili Kinga mazao kwa kutumia njia za kiutamaduni mfano, weka shamba katika hali ya usafi,tumia mbegu inayokinzana na nondo wa k**a zipo, kilimo cha kubadili mazao au kupanda mimea inayozuia wadudu wasiingie shambani Ondoa masalia ya mimea ya mimea baada ya kuvuna na choma moto Tumia mitego yenye mtego wa maji yenye harufu ya kipepeo jike, hivyo kuwa na uwezo wa kuvutia madume na mara yanapoingia yanakufa.





VIUADUDU VINAVYOWEZA KUDHIBITI KIWAVIJESHI VAMIZI

Alpha-cypermethrin 10EC (systemic)lambda-cyhalothrin 5 SC au 100CS (Contact)Indoxacarb 14.5 EC au 150 EC/SL

04/05/2022

Nikiwa katika utafiti binafsi nimegundua jambo moja. Baadhi ya Wakulima wetu wanalima na technology ya enz hizo kitu kinachowafanya waendelee kuoata matokeo wanayopata sasa na kukalamika kilimo ni pata potea. Nilishasema na nitazid kusema.
KILIMO NI SAYANSI HALISI, SIO SIASA NA PROPAGANDA ZINAZOSEMA KILIMO NI PATA POTEA.
Ziko sababu kwanini hatufiki. Na moja wapo ni BAADHI YA WATAALAMU WETU KUTOKUA NA ELIMU YA UZALISHAJI NA KUA NA ELIMU YA KUNADI PEMBEJEO KIBIASHARA.
TUNAKUJA KUKUFUNGULIA FUMBO HILI.
ENEO DOGO MAVUNO MAKUBWA.
Hitaji letu ni kufikia kila mkulima kwa njia yeyote ile. Niwakaribishe kwa maswali na maoni.
Tukumbuke pia kipanda miti ya matunda na ya kawaida ni jambo muhimu kwa kutunza mazingira dhidi ya mabadiliko yabtabia nchi yanayotutesa wakulima kwa kiasi fulani.
Join together for better education

Photos from FAPRO NGO's post 12/12/2020

Huduma ya ushauri wa kitaalam kwa wakulima na ufugaji wa kuku unazidi kutolewa. Karibuni nyeto kwa wale wa moshi.
Kwa nje ya moshi group la wasap litafunguliwa kesho jumapil jion.
Yajayo yanafurahisha

Want your business to be the top-listed Business in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Ushirika
Moshi