Maguge Tv

Maguge Tv

Share

This page is describe product from Maguge Media and defferent product found on maguge media Maguge Media

25/07/2022

"Chanzo cha Yanga SC kucheza bila mashabiki dhidi ya Rivers Utd, ni (TFF).

"Mchezo wetu na Rivers United (TFF) chini ya katibu mkuu kidao na Rais wa (TFF) Wallace Karia, hawakuomba kwa maandishi (CAF) k**a sisi tulivyowaomba (TFF) tupate idhini ya kuingiza mashabiki kwenye mechi dhidi ya Rivers 🇳🇬, wakaandika barua nje ya muda"

"Kipindi hicho Karia kwa siku anapiga simu tatu, Kidao simu nne ili nipoze hilo jambo (Nisiseme) na nilifanikiwa"

"Hatukucheza tukiwa na mashabiki uwanjani dhidi ya Rivers kwa sababu ya (TFF)" - Haji Manara, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.

25/07/2022

‘Barbershop,’ ambazo mbali na kuwanyoa nywele kichwani wateja, pia huwasinga sehemu mbalimbali za mwili (massage).

Mwandishi wa habari hii amefuatatilia huduma hiyo kwa siku kadhaa katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Awali, akizungumza na mwandishi kuhusu yanayotendeka ndani ya saluni za kisasa, Israel Joachim anasema, “niliwahi kwenda saluni, lengo halikuwa kunyoa nywele, bali nifanyiwe ‘massage,’ kweli nilifanyiwa tena na msichana, haikuwa rahisi kuvumilia, kuna maeneo hatarishi nilikuwa nashikwa na huyo dada akaniambia k**a hali ni mbaya nijiongeze.”

Anasema baada ya kuingia kwenye saluni hizo kupata huduma, alichokutana nacho, hakimtoki kichwani kwa kuwa mbali na kulainisha misuli na kupunguza uchovu, vyumba vilivyomo saluni vina ushetani mwingi.

“Nilijiuliza nijiongeze na nini, kumbe alitaka (mtoa huduma mwanamke) nimpatie Sh30,000 anisaidie kuondoa hali niliyokuwa nayo, sikuwa na ujanja, nilitekeleza takwa lake sababu sikuwa na la kufanya kutokana na hali yangu,” anasema Joachim.

Hata hivyo, Mwandishi alibaini baadhi ya vyumba hivyo ni kichaka kipya cha biashara ya ngono na inaelezwa asilimia 80 hadi 90 ya wanaume wanaokwenda huko hufuata huduma hiyo ya ngono, ingawa huzuga kwa kuanza kwanza na huduma ya ‘massage.

“Wanaanza na huduma ya kwanza kwa sababu ile ya pili hawana uhakika k**a inatolewa pale, kwa baadhi ya watu niliowauliza kwa nini wanakwenda kule wanasema wale wanawake wanaotoa huduma hizo wana uwezo mkubwa wa kuwaandaa wanaume kushiriki ngono,” alisema Ramadhani Masenga, mtaalamu wa saikolojia kutoka Mental Health Hygiene Institute ya Dar es Salaam.

23/07/2022

Katika mahojiano na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amegusia suala la “Tumbili” lililozua mvutano kati ya Jaji Warema na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila Juni 2014.

Jaji Warema amesema kuwa alitumia msemo huo wa Kiganda kueleza kuwa ukiwa jikoni ndivyo unavyoweza kubaini mambo,

"Tumbili haamui mambo ya msituni" mimi ndio nilikuwa jikoni najua kilichokuwa kinaendelea, kwa hiyo kutumia neno tumbili ni Msemo ila watu walitafsili vibaya tu sikuwa na maana ya kumtukana binadam mwenzangu aliyeumbwa na Mungu.

20/07/2022

Huko nchini Uingereza😲 Mapya yaibuka! Mwanadada kwa jina la Charlotte(23) amelazimika kununua mdoli wa mapenzi unaofanana nae ili uweze kumsaidia katika mahusiano yake kwani bwana'ke huyo kwa jina la Callum(28) kiwango chake cha kufanya mapenzi kipo juu tofauti na yeye hapendi sana hivyo kushindwa kuhimili mechi za kibabe toka kwa bwana'ke huyo.

Charlotte amesema awali hakuafiki suala la kuruhusu mdada mwingine aingie katika mahusiano yao wawe katika mahusiano ya utatu sababu yeye angesikia wivu k**a ilivyo kwa watu wengi.

Hivyo, ilibidi aongee na bwana'ke huyo wanunue mdoli anayefanana nae awe anamsaidia 'kazi' pale anapokuwa hajisikii huku bwana'ke anataka. Ameongeza kwamba sababu ni mdoli wa plastiki hatosikia wivu tofauti ingekuwa ni mdada mwenzie kikwelikweli angejisikia wivu na kuleteana gubu.

Na ndio wakanunua hilo doli mwezi June mwaka huu kwa pesa ndefu, wanalivalisha nguo za kuvutia, pia wanalitoa out kwa gari doli hilo kwenda kutembea huku na huko ili lisijihisi upweke au kutengwa ndani na nje ya nyumba.

Charlotte anadai tangu hapo anahisi mahusiano yao yapo salama na yamenogeshwa na doli hilo.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Bugarika Pamba Nyamagana Mwanza
Mwanza
BUGARIKA,33214