KuniSMART
Kuni za Kiwandani: ni ZAIDI ya mkaa na kuni za kawaida. Joto jingi, hazina moshi na zinapika kwa HARAKA. Zina GHARAMA NAFUU kwa Mapishi ya Shuleni au Nyumbani.
Mara nyingi, clean cooking huonekana k**a kitu cha gharama kubwa—lakini je, ni lazima iwe hivyo?
Hivi karibuni tumekamilisha ufungaji wa jiko la taasisi la kuniSMART (lililojengwa kwa matofali) katika shule moja binafsi ya hapa nchini. Kilichojitokeza wazi ni kwamba, inawezekana kabisa kuhamia kwenye clean cooking kwa gharama nafuu zaidi kuliko wengi wanavyodhani.
Chabri Energy, tunabuni suluhisho kwa kuzingatia uhalisia wa watumiaji. Mradi huu ulituhitaji kutoa jiko lenye ufanisi mkubwa, linalokidhi mahitaji ya upishi wa taasisi, huku likibaki ndani ya bajeti ndogo ya shule. Matokeo yake ni jiko linalotumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi hapa nchini, lenye matumizi madogo ya kuniSMART, na linalodumu kwa muda mrefu.
Lakini swali muhimu ni hili:
Kwa nini bado clean cooking unaonekana kuwa wa gharama kubwa, wakati suluhisho nafuu tayari zipo?
Kwa shule na taasisi:
Ni changamoto gani kubwa inawazuia kuhamia kwenye clean cooking?
Je, ni gharama ya kuanzia, uelewa, au imani juu ya teknolojia hizi?
Kwa wadau na wataalam wa sekta hii:
Tunawezaje kupanua matumizi ya suluhisho k**a hili bila kuongeza gharama?
Ni mifumo gani mmeona ikifanya kazi vizuri katika mazingira k**a haya?
Tunaamini mjadala unapaswa kubadilika—kutoka “clean cooking ni ghali” hadi “tunawezaje kuufanya clean cooking ipatikane kwa wote?”
Ningependa kusikia mawazo na uzoefu wenu.
kuniSMART
13/03/2026
On 12th March 2026, the British Deputy High Commissioner, Sally Hedley, paid an official visit to the offices and factory of Chabri Energy Ltd to gain insight into the company’s operations and its role in advancing sustainable energy solutions in Tanzania.
26/01/2026
kuniSMART biomass briquettes ni aina ya nishati safi inayotokana na mabaki ya mimea (biomass) k**a vile mabaki ya kilimo, maganda ya mazao, vumbi la mbao, au taka za misitu. Mabaki haya hukandamizwa kwa teknolojia maalum bila kemikali, na kutengeneza briquettes zenye msongamano mkubwa na uwezo mzuri wa kutoa joto.
K**a nishati safi, kuniSMART biomass briquettes zina sifa kuu zifuatazo:
Kwanza, zina ufanisi mkubwa wa nishati. Briquettes huwaka kwa muda mrefu na kwa joto thabiti kuliko kuni za kawaida, hivyo kupunguza kiasi cha nishati kinachohitajika kwa matumizi ya kupika au shughuli za viwandani.
Pili, zinachangia kupunguza ukataji wa miti. Kwa kuwa zinatengenezwa kutokana na mabaki ya biomass badala ya miti hai, matumizi yake husaidia kuhifadhi misitu na kulinda mazingira.
Tatu, zina uchafuzi mdogo wa hewa. KuniSMART briquettes hutoa moshi kidogo na chembechembe chafu (particulate matter) kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na kuni au mkaa wa kawaida, hivyo kuboresha afya ya watumiaji na mazingira ya ndani.
Nne, ni nishati endelevu na rafiki kwa mazingira. Biomass ni rasilimali inayoweza kurejeshwa, na matumizi ya briquettes husaidia kupunguza taka za kilimo na viwandani ambazo vinginevyo zingesababisha uchafuzi.
Mwisho, kuniSMART biomass briquettes ni mbadala wa gharama nafuu kwa kuni na mkaa wa kawaida, hasa kwa kaya, taasisi, na biashara ndogo, huku zikisaidia mpito kuelekea matumizi ya nishati safi na endelevu.
Kwa ujumla, kuniSMART biomass briquettes ni suluhisho la kisasa la nishati safi linalounganisha ufanisi wa nishati, uhifadhi wa mazingira, na ustawi wa afya ya jamii.
12/01/2026
We are happy to have Anina as part of our team. Since joining Chabri Energy, she has become part of our work to provide clean and affordable energy solutions to communities.
We appreciate having her with us and look forward to working and growing together. Welcome to the team, Anina!
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Kisesa
Mwanza
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| Wednesday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| Friday | 09:00 - 17:00 |
| Saturday | 09:00 - 17:00 |