Famara Media

Famara Media

Share

Famara Media - Inform, Entertain and Educate.

02/06/2026

📢 tunaungana na Watanzania wote kuisapoti katika mchezo wa Fainali dhidi ya Senegal leo.

Tukiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , tumeungana katika kuwapa hamasa na nguvu vijana wetu wanaoiwakilisha Tanzania katika hatua hii muhimu.

Tunawatakia kila la heri Serengeti Boys. Pambaneni kwa moyo, nidhamu na uzalendo. Tanzania ipo nyuma yenu na inaamini katika uwezo wenu.

🇹🇿⚽ Mshik**ano wetu ni nguvu yao, ushindi wetu ni fahari ya Taifa.

01/06/2026

Ujenzi wa Uwanja wa Kisasa wa Arusha unaoendelea chini ya Serikali ya Tanzania umefikia hatua za kuridhisha, jambo linaloonyesha dhamira ya nchi kujiandaa kwa mafanikio kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Mradi huo mkubwa wa kimkakati unalenga kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa kwa viwango vinavyokubalika na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Uwanja huo unatarajiwa kuwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika wakati wa AFCON 2027, ambayo Tanzania itashirikiana kuandaa pamoja na Kenya na Uganda.

Picha za maendeleo ya ujenzi zinaonyesha kazi mbalimbali zikiendelea kwa kasi, ikiwemo uwekaji wa miundombinu ya msingi, maeneo ya watazamaji na huduma nyingine muhimu zinazohitajika katika uwanja wa kisasa.

Kukamilika kwa mradi huo kutaleta manufaa makubwa kwa sekta ya michezo, utalii na uchumi wa Mkoa wa Arusha, huku ukifungua fursa zaidi za ajira na biashara kwa wananchi wa eneo hilo.

Maendeleo hayo yanaendelea kuwapa matumaini Watanzania wengi wanaosubiri kuona nchi yao ikiandika historia kwa kuwa sehemu ya waandaaji wa AFCON 2027, mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika.

31/05/2026

KWANINI ARSENAL INACHUKIWA?

Mashabiki wa Arsenal wameendelea kuhoji sababu za kuonekana kwa upinzani mkubwa kutoka kwa mashabiki wa timu nyingine baada ya mafanikio ya klabu hiyo.

Baadhi yao wanaamini kuwa ushindani huo umeongezeka kutokana na Arsenal kurejea katika kiwango cha juu na kusherehekea mafanikio yake kwa nguvu.

Wanasema hawana tatizo na timu nyingine, bali wanaona ni kawaida kushangilia mafanikio makubwa k**a ubingwa wa EPL.

Huku wakitazama mbele, mashabiki wa Gunners wana matumaini kuwa usajili mpya, maandalizi bora na mbinu sahihi zitaiwezesha timu yao kufanya vizuri zaidi na kuwania taji la UEFA msimu ujao.

"Mafanikio si bahati, ni matokeo ya mipango na mikakati sahihi.

🔴⚪️🏆

Want your business to be the top-listed Media Company in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Nyamagana
Mwanza
994