George Kabadi

George Kabadi

Share

Mchambuzi Wa Siasa

05/09/2025

DIAMOND NI KITABU CHA MKOSA FADHILA HAKIWEZI KUANDIKA SHUKRANI.

Na George Kabadi

Mafanikio ni sawa na Madaraka, Madaraka yanalevya na Mafanikio yanalevya ni vileo ambavyo ukiruhusu vikuongoze badala ya kuviongoza unaweza kuua mke, watoto na wazazi wako ili kuimarisha himaya yako.

Mungu humwinua mtu kupitia watu na humbariki mtu kupitia watu, haiwezekani kuwa binadamu ukawa kiongozi wa mawe na haiwezekani kuwa mwanamuziki mwenye ndoto za kuwaimbia ng'ombe, na katika ndoto zako ukatarajia kupokea mafanikio ya ng'ombe kuja kwenye SHOW zako kwa kulipa viingilio na kupakua nyimbo zako mtandaoni; HAIWEZEKANI! Mtu kufanikiwa pasipo na watu.

Kuna wanaofanikiwa na wanafanikiwa kurudisha fadhila kwa jamii zao kwa sababu wanaelewa mchango wa anayekukatisha tamaa na anayekutia moyo ni muhimu kuliko mchango wa aliyekaa kimya katika harakati zako na kuna wanaofanikiwa na wanafanikiwa kulewa na mafanikio, hawa hata Mungu aliyewapa mafanikio kupitia watu humkosoa, Mtu alikuwa Mwanaume atataka kuwa mwanamke; NDIYO! atafanya yale yanayompendeza yeye na si yaliyowapendeza watu nyakati za kuinuliwa kwake.

DAIMODI amekosa fadhila, anasahau anaowatukana na kuwadhihaki baada ya kulewa na mafanikio, ndiyo waliyokuwa wanahudhuria SHOW zake, wakati hajui kuoga vizuri, ndiyo waliyokuwa wanauza vitumbua na kubeba zenge ili wapate bando la kuingia mtandaoni na kupakua nyimbo zake. Dunia haijawahi kumsaliti mtu, bali mtu husalitiwa na mtu.

Kioo cha Jamii ya Watu, Kimegeuka kuwa Toilet paper ya Choo cha Stendi ya wanasiasa.

George Kabadi


Nakala.

07/06/2025
26/10/2023

Jenga Jengo lako na Kampuni bora kabisa ya Ujenzi ya KABADI Construction. Tuna mafundi bora waadilifu na wabunifu. Piga 0746443295 au 0652265757

26/10/2023

Nilipata bahati ya kubadilishana fikra na Baba Askofu Stephen Munga PhD wa KKKT pamoja na Mhe: Magenzi Mkandala. Tunapaswa kujifunza zaidi

Want your organization to be the top-listed Government Service in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Misungwi
Mwanza