Mwauwasa
Ukurasa rasmi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)
Kwa msaada piga simu namba (0800110023) BURE
30/05/2026
KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MWAUWASA YAANZA KWA VITENDO
Katika kuungana na wadau kuhakikisha na kuhamasisha umuhimu wa usafi wa mazingira, Watumishi wa MWAUWASA wameungana kufanya usafi kwenye maeneo ya vyanzo vya maji kikiwemo chanzo cha Butimba.
Hatua hiyo ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya usafi wa Mazingira ambayo huadhimishwa tarehe 5 ya kila mwaka Duniani kote.
Siku ya Mazingira Duniani (World Environment Day), Iliwekwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 kwa lengo la kuongeza uelewa na kuhamasisha hatua za kulinda mazingira duniani.
Kwa Mwaka huu Tanzania inaadhimisha siku hiyo kwa kaulimbiu isemayo "Dira 2050, Tuwajibike Kukijanisha Tanzania"
18/05/2026
Katika kuadhimisha Siku ya Ziwa Victoria, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, leo Mei 18, 2026 wameungana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda pamoja na viongozi wengine wa serikali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Bi. Rose Ambrose kupanda zaidi ya miti 2,000 katika chanzo cha maji Butimba. Zoezi hili linaongeza idadi ya miti iliyokwisha pandwa kufikia zaidi ya 6,500 katika eneo hilo muhimu.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa Said Mtanda aliwapongeza wananchi na wadau mbalimbali kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika juhudi za uhifadhi wa mazingira. Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda rasilimali za maji, hususan Ziwa Victoria ambalo lina mchango mkubwa katika maisha ya watu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa kwa mwaka huu, maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria yamefanyika kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo wakuu wa nchi na mawaziri wa sekta za maji na mazingira walikubaliana kuwa na siku maalum ya kuenzi na kulinda ziwa hilo.
“Ziwa Victoria ni muhimu sana kwa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Maji ni afya, maji ni uchumi na maji ni maendeleo,” alisisitiza Said Mtanda huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanatunza miti iliyopandwa ili iweze kudumu na kutoa manufaa yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bi. Rose Ambrose, alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki kikamilifu katika tukio hilo, na kupongeza juhudi za wadau wote wanaoshiriki katika uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Aliongeza kuwa Wizara ya Maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imejiwekea lengo la kupanda miti 10,000 rafiki kwa vyanzo vya maji katika eneo la Butimba, ambapo hadi sasa miti zaidi ya 6,500 tayari imepandwa.
Miti iliyopandwa inalenga kulinda vyanzo vya maji, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha mazingira kwa ujumla katika eneo la chanzo cha Butimba.
Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo: “Maji yetu, mustakabali wetu – tuungane kwa uendelevu wa Bonde la Ziwa Victoria.”
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Telephone
Website
Address
P. O. Box 317
Mwanza
255
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 17:00 |
| Tuesday | 08:00 - 17:00 |
| Wednesday | 08:00 - 17:00 |
| Thursday | 08:00 - 17:00 |
| Friday | 08:00 - 17:00 |
| Saturday | 08:00 - 18:00 |