ELCT - ELVD

ELCT - ELVD

Share

East of Lake Victoria Diocese (ELVD) is part of the Lutheran Church in Tanzania (ELCT).

Photos from ELCT - ELVD's post 17/05/2026

Baba Askofu Oscar I. Lema leo Mei 17, 2026 ni miaka 37 ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria amehudumu kwa njia ya mahubiri katika Usharika wa Imani Kanisa Kuu.
Askofu amesisitiza wakristo juu ya kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu na kutumika ili kumfata Kristo
Katibu Mkuu wa KKKT Bwana Rogath Mollel ameshiriki ibaada hii na kutoa salamu kutoka KKKT Makao Makuu.

Photos from ELCT - ELVD's post 10/05/2026

UZINDUZI WA JIWE LA MSINGI MTAA WA REHOBOTH-ILALILA

Baba Askofu Oscar I. Lema leo Mei 10, 2026 ameweka jiwe la msingi katika Mtaa wa Rehoboth-Ilalila. Mtaa huu unatunzwa na Usharika wa Imani Kanisa Kuu.
Askofu Lema amewahasa wakristo wanapaswa kumuomba Mungu siku zote k**a sala ya Bwana inavyoelekeza na sio kupayuka payuka na watu waendelee kufanya kazi ya Mungu kwa kujitoa kwa moyo.
Mtaa wa Rehoboth-Ilalila ina jumla ya washarika sitini (60).
Makamu Mkuu wa Chuo cha Biblia Nyakato Mchg. Mimi Brown amepata nafasi ya kuwakaribisha wakristo wote wanaopenda kusoma na wenye watoto, ndugu, jamaa na marafiki wajiunge na Chuo chetu kinachotoa kozi ya maendeleo ya jamii kwa ngazi ya cheti na diploma.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


P. O. Box 423
Mwanza