NUMET

NUMET

Share

Workers' Union

23/09/2025

Mwanzoni nilikuwa siamini k**a karne hii ,bado tuna maafisa rasilimali watu (HR Officials) wenye akili za kikaburu za kuzuia wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

Lakini leo nimepokea kisa kimoja kutoka kwa makampuni mawili Tofauti, ambapo tatizo linafanana.

Viongozi wa chama cha wafanyakazi wameomba fursa kwa mujibu wa sheria, kuongea na wafanyakazi ili kuwashawishi waungane pamoja waweze kuwa na sauti moja ya , na haki na masilahi yao.

Baada ya vikao kadhaa vya wafanyakazi na viongozi wa chama, wanachama wanaamua kujiunga na chama.

Afisa rasilimali watu anaibuka kutoka kusikojulikana , anasema hawezi kukata ada za uanachama kwenye mishahara yao eti anahisi wafanyakazi hawakupata elimu ya kutosha?

Sasa unajiuliza ametumia kigezo gani? Je, aliamini wakipata elimu watakataa kujiunga na sasa anashangaa kwanini wamejiunga?

Je , kuna cheti cha kufuzu anapaswa kupewa mfanyakazi kabla ya kujaza fomu ya TUF 15 iliyotolewa na sheria?

Ni kwanini sisi watanzania tuliopewa dhamana tunaona fahari kuwakwamisha waliochini yetu?

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Mwanza