HEALTH PLANET
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from HEALTH PLANET, Biotechnology company, Mwanza.
24/01/2022
KIPIMO KINACHOSAIDIA KUJUA SIKU ZA KUSHIKA UJAUZITO.
💥Mwanamke hushika ujauzito kipindi anapokuwa amepevusha mbegu ya k**e, Upevushaji wa mbegu ya k**e yaani ovulation hutokea katika siku za katikati za mzunguko wa hedhi, kati ya siku ya 12 hadi 16 kwa wanawake walio wengi ambao huwa na mzunguko wa siku 28.
💥Wakati wa kipindi cha upevushaji joto la mwili,uteute mzito kwenye via vya uzazi, na hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Wanawake walio wengi hushindwa kubaini mabadiriko haya na kupita kwenye kipindi hiki bila kujua.
💥Pamoja na hivyo mzunguko wa hedhi unaweza kuwa tofauti kati ya mwanamke mmoja na mwingine, unaweza kuwa na idadi ya siku tofauti kati mwezi mmoja na mwingine au upevushaji kutokea siku tofauti tofauti kati ya mizunguko kila mwezi.
💥Hali hii husababisha mwanamke anaetaka kupata ujauzito kushindwa kujua au kupatia kipindi sahihi cha mbegu ya k**e inapopevuka ili ajiandae kushika ujauzito.
👉Kipimo cha kubaini kipindi cha kushika ujauzito hufahamika kitaalam k**a Ovulation test kit au Ovulation Predictor kit(OPK), Hupatikana kwenye maduka makubwa ya dawa(pharmacy)
👉👉👉Hupima uwepo wa homoni ya LH ambayo huongezeka mwilini masaa 12 hadi 36 kabla ya kupevusha mbegu ya k**e.
👉👉👉Kipimo cha strip(utepe) hufanana na kipimo cha ujauzito, hupimwa kwa kutumia sampuli ya mkojo, majibu husomwa kwa kuangalia mistari inayochora kwenye utepe baada ya kuuchovya kwenye mkojo.
👉👉👉Kina uwezo asilimia 97 wa kuonesha majibu sahihi. Majibu chanya huashiria aliepimwa atapevusha mbegu ya k**e baada ya masaa 12 hadi 36.
👉👉👉Mtumiaji huitaji kuanza kupima siku chache kabla ya kufika katikati ya mzunguko wake, kwa mzunguko wa kawaida wa siku 28, huanzia siku ya 10.
💥Baada ya kusoma majibu chanya, mtumiaji atahitaji kushiriki tendo la ndoa kuanzia siku aliyopata majibu chanya na kuendelea angalau kwa siku 3 ili kuongeza uwezekano wa kushika ujauzito.
💥Kipimo hiki hakisaidii kwa wanawake wenye mzunguko wa hedhi uliovurugika ambao hauna mpangilio sahihi wa kuelewa mwanzo kati na mwisho, hakisaidii kwa wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya yanayosababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito.
💥💥Kwa ushauri zaidi, Karibu
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mwanza