AFYA Kwanza

AFYA Kwanza

Share

Karibu kwenye ukurasa huu kupata suluhisho la Magonjwa sugu yasioambukizwa

04/05/2023

Tibia chanzo cha tatizo

30/04/2023

UMUHIMU WA MADINI YA CALCIUM MWILINI. DR.DAVID

Calcium husaidia afya ya mwili kwa njia nyingi. Baadhi ya kazi za calcium katika afya ya binadamu ni k**a:

Afya Ya Mifupa

Karibu asilimia 99 ya calcium ya ndani ya mwili ipo ndani ya mifupa. Calcium ni ya muhimu katika kujenga, ukuaji na ukarabati wa mifupa.

Watoto wanapokua, calcium huchangia ukuaji wa mifupa yao. Wakiacha kukua, calcium husaidia kuitunza mifupa na kupunguza kasi ya kupungua kwa uzito wa mifupa, hali ambayo huambatana na kuzeeka kwa mwili.

Wanawake waliokoma hedhi wanaweza kupunguza uzito wa mifupa haraka zaidi kuliko wanaume au vijana, kwa hiyo daktari anaweza kuwashauri watumie calcium ya ziada.

Kukaza Kwa Misuli

Calcium inasaidia kudhibiti kukaza kwa misuli. Neva ikiusisimua msuli, mwili huachia calcium. Calcium huzisaidia protini za ndani ya msuli kukamilisha tendo la kukaza. Mwili ukiisukuma calcium nje ya msuli, msuli hujilegeza.

Afya Ya Moyo

Calcium inahusika katika kuganda kwa damu. Tendo la kuganda kwa damu ni gumu kulielezea na lina hatua kadhaa. Ni tendo linahusisha mabadiliko kadhaa ya kikemikali, calcium ikihusika.

Kuhusika kwa calcium katika utendaji kazi wa misuli ni pamoja na kazi za msuli wa moyo. Calcium huulegeza msuli unaozunguka mishipa ya damu. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kwamba kuna mahusiano kati ya ulaji mkubwa wa calcium na tatizo la kuwa na msukumo mdogo wa damu (low blood pressure.)



Nini Kitatokea Ikiwa Calcium Ipo Chini Katika Mwili?


Upungufu wa calcium, kitaalamu hypocalcemia, unatokea pale kiwango cha calcium katika damu kinapopungua. Upungufu wa calcium katika damu wa muda mrefu husababisha matatizo ya meno, mtoto wa jicho, mabadiliko katika ubongo na mifupa kukosa uimara.

Dalili Za Upungufu Wa Calcium

Matatizo ya Misuli

Mtu mwenye upungufu wa calcium anaweza kuona:
kuumwa kwa misuli, kabanwa misuli (cramps), misuli kucheza Maumivu kwenye mapaja na mikono wakti wa kutembea Ganzi na vitu kuchezacheza kwenye mikono, miguu, nyayo na kuzunguka midomo

Dalili hizi zinaweza kuja na kutoweka
Mtukutiko wa maungo (kwa kifafa, dege),
Mapigo ya moyo kwenda kasi au taratibu (arrhythmia)
Kifo

Uchovu Mkubwa

Viwango vidogo vya calcium husababisha uchovu mkubwa, unaotokana na kukosa nishati. Tatizo la kukosa usingizi pia linaweza kutokea. Uchovu unaotokana na upungufu wa calcium unaweza kuambatana na kichwa kuwa chepesi, kizunguzungu au kichwa kizito -vinavyoweza kusababisha kukosa umakini, usahaulifu na kuchanganyikiwa.

Matatizo Ya Ngozi na Kucha

Upungufu wa calcium wa muda mrefu unaweza kusababisha:
ngozi kavu kucha kavu, zinazovunjikavunjika nywele kavu alopecia, tatizo la nywele kupunyuka vifunguvifungu eczema, uvimbe wa ngozi unaoweza kusababisha miwasho au madoa ya ngozi kavu Psoriasis

Mifupa kupoteza uimara

Upungufu wa calcium wa muda mrefu husababisha kupotea kwa ujazo wa madini (osteopenia) hali ambayo itasababisha mifupa kupungua unene na kuweza kuvunjika kirahisi, maumivu na matatizo ya mkao wa mwili (body posture.)

Maumivu Makali Kabla Ya Hedhi (Severe PMS)

Kiwango kidogo cha calcium katika mwili kimehusishwa na maumivu makali ya kabla ya hedhi. Utafiti umeonyesha kuwa upungufu wa vitamin D na calcium katika kipindi cha pili cha mzunguko wa hedhi unachangia dalili za PMS.

Matizo Ya Meno

Mwili ukipungukiwa calcium, huchukua calcium kutoka mwilini ikiwa ni pamoja na kutoka kwenye meno. Hii huweza kusababisha matatizo kwenye meno, yakiwa ni pamoja na:
meno kuoza meno kuvunjika matatizo ya fizi udhaifu wa mizizi ya meno

Upungufu wa calcium kwa mtoto mdogo huathiri ukuaji wake wa meno.

Mfadhaiko

Ushahidi mwingine unasema upungufu wa calcium unaweza kuhusishwa na mabadiliko ya hisia za mwili, pamoja na mfadhaiko.



Chakula Chenye Calcium Kwa Wingi


Watu wanaweza kupata calcium kutokana na chakula na vinywaji vya aina nyingi:
mtindi maziwa sardine na salmon jibini tofu mboga za kijani, k**a broccoli, turnip, kale n.k. nafaka katika mlo wa asubuhi juisi mbegu k**a almonds, ufuta na chia jamii ya kunde.



Supplements Za Calcium


Daktari anaweza kushauri matumizi ya supplements kwa watu wenye upungufu wa calcium. Supplements nyingi za calcium zina vitamini D. Vitamini D husaidia mwili kufyonza calcium. Magnesium pia ina nafasi katika kuimarisha mifupa, hivyo supplements za calcium zinaweza kuwa na magnesium.

30/04/2023

**CHANZO CHA TATIZO* LA *UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME*

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri.
Kuna *mitindo ya maisha* inayoweza kukuweka *hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni* pamoja na;

💎 *Kuwa na halemu* (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo
💎 *Kuvuta sigala na* unywaji wa pombe
💎 *Uzito kupita kiasi na* unene uliozidi
💎 *Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta* mengi na sukari nyingi
💎 *Kisukari*
🎙️ *Kuwa na mawazo na wasiwasi*
🎙️ *Matumizi ya madawa* *mbalimbali*
🎙️ *Umri hasa wazee*
🎙️ *Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili*
🎙️ Kuwa na tatizo la kibofu
🎙️ *Tabia za kujichua kwa* mda mrefu
🎙️ *Kutopata usingizi kamili*
🎙️ *Matumizi makubwa* ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa k**a kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine

Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Njombe