Simulizi Zetu

Simulizi   Zetu

Share

Mtunzi Wetu

22/09/2021

MOYO WA MASIKINI sehemu ya PILI

simulizi zetu page njombe Tanzania

inaendelea

kibasu aliondoka kwa hasira binti akiwa kazubaa , kiba anafika nyumbani anamkuta mdogo wake yupo nje amekaa ameshika shavu ,

" mama yupo wapi?"

zaru " yupo ndani kapumzika , amechoka na harusi "

" sawa Mimi nataka nikalale nipumzike akija mtu yeyote yule mwambia sipo"

zaru " hayaa hata Dada ADA ?"

"ndio mwanbie sipo"

kiba aliingia ndani na kupumzisha hasira huku moyo wake ukiwa umejaa hasira anakumbuka maneno makali ya yule mama ,anahisi kupasuka

ASUBUHI NA MAPEMA __ kiba anagongewa mlango na mdogo wake " zaru"

" kaka kumekucha huendi shambani niandae chakula"

KIBA " siendi mama kaamka salaam "

" ndio kaenda kuchimba viazi "

KIBA " haya Leo Mimi tunashinda wote"

kiba aliamka akijinyoosha nyoosha viungo anafungua mlango wa chumba chake na kuingia sebuleni anachukua kikombe cha maji anazunguka nyuma ya nyumba , kabla ya kuanza kunawa maji anamsikia ADA anamsema mdogo wake

" wewe zaru kiburi kimeanza lini hata salamu , wala kunipa Kiti"

ZaRu " shikamoo , "

"kaka yako yupo wapi "

zaru alikaa kimya hakuwa anataka kumjibu alimuangalia K**a hajamsikia vile ADA alikasilika anataka kuondoka anakutana na mama zaru "mjane"

" umefuata nini mwanangu "

ADA "shikamoo, nilikuwa na shida na kiba "

"Zaru kaka yako yupo WAP"

ZARU " sijui mama , kaka kaenda wapi "

" sawa , na wewe ADA uje baadae saiz hayupo halafu nitakuwa na mazungumzo na we we"

ADA " sawa mama"

ADA anaondoka kiba aanatokea nyuma ya nyumba na kikombe chake mswaki mkononi , akamsalimia mama yake ,mama alikuwa anamshangaa kiba bila kujali aliingia ndani akatoka nje moja kwa kwenye mfuko aliyo beba mama yake akachukua kiasi kimoja kabla hajainuka alipigwa kofi na mama yake

".mmmmmh mama"

MAMA " pumbavu wewe unaacha kusubiri tupike wewe unatafuna vibichi ukiumwa tumbo halafu hujuii utapata minyooo"

" ngoja sasa mama najua umekasirika sio kiazi ila kuhusu ADA "

MAMA "hata ungekuwa wewe baba yako siku ile shambani ulipo kula chakula bila kumjali yeye alikuambiaje nilikuwepo ujue , alikuambia katika maisha yako usijalibu kumfanyia mtu kitu chochote ambacho wewe hupendi kufanyiwa "

" sawa , ila mama samahani siitaji kuongea Sana k**a wewe ulipenda kuzalilishwa na mama yake Sababu yeye mimi hapana "

MAMA" hallo , litoto wewe sijui nikupeleka wapi aah"

" nipeleke china nikaone magorofa makubwa marefu k**a ubongo wangu , ZARU mdogo wangu mama ananjaa mpikie ale mimi naenda kwa kina AZA "

MAMA " asubuhi Unaenda kwa watu kufanya nn k**a kuku vile"

kiba aliondoka wakati huo mama yake alikuwa akiongea pekee yake "

ADA akiwa njiani anaenda nyumbani alikumbuka aliagizwa sukari aliona bora akanunue kabisa asije akasahau wakati anavuka barabara ya gari

" barabara ambayo walichimba wananchi kwa jembe ya mkono kutokana na kuzawadio gari na mbunge kwa kuweza kulima chakula kingi ambacho kililisha wilaya nzima , mazao yalikuwa yanasafirishwa kupitia gari la zawadi pamoja na kuwasafirisha wagonjwa kwa hiyo 60% ya wanakijiji wanajua dunia nzima kuna gari moja tu ambalo walipewa zawadi "

Alikuta gari lingine ambalo ni jeusi la gharama balaa alisimama kulishngaa nalo gari likasimama

" ADA MAMBO "

ADA " AYUNI umerudi aah hallo mungu mkubwa "

" njoo hapa sasa , umekuwa mrembo mmmh npe namba ya simu"

ADA " simu !!!!!!!??????? haha hah hahaha"

" hahha na Mimi nilijua nipo mjini "

ADA " KIBA alikuwa anakusubiri "

" ndio naenda kwake kwanza kabla ya kwenda kwa Bibi yang u"

waliachana kihivyo Ila AYUNI alitokea kumpenda sana kwa ADA alivutiwa mazima ,AYUNI akutembea kitambo kirefu alimkuta kiba njiani alipiga oni kiba alishtuka kwa hasira aliokota jiwe alizani kitu gani hicho chenye matairi K**a gari LA kijiji AYUNI alifungua mlango akamwita kinyaru " kipaka " kiba alijikuta anaangalizia meno , hakuamini rafiki yake karudi toka aachane miaka 5 hivi alibeba fimbo

" acha utani kiba fimbo hiyo "

KIBA " kwanini uje bila taarifa , tungekuandalia hata mbizi "

" ndio nimekuja Ila nitakaa siku 3 Ila nitaenda mjini na wewe ukale maisha

SAMAHANI NI FUPI SABABU SINA MUDA WA KUTOSHA KUCHAPISHA ILA HAKIJA HARIBIKA KITU CHONDE NAOMBA SAPORT MNISAIDIE KuSHARE HATA KIKUNDI KIMOJA ANamgalau coment na like bila kusahau

page"

Want your business to be the top-listed Engineering Company in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Njombe