Kings FM Radio
đź”»Tunagusa Kila nyanja unayotamani kuisikiađź‘‚89.5-Njombe đź”»www.kingsfm.co.tz Chaugingi Street:
Njombe, Tanzania. http://tunein.com/radio/Kings-FM-1043-s263641/
08/05/2026
Shirika la umeme Tanzania Mkoa wa Njombe limetangaza kusitisha huduma ya umeme kwa muda katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Njombe kutokana na kazi za matengenezo kinga na maboresho katika kituo cha kupoza umeme cha Makambako (Substation).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, zoezi hilo litafanyika kesho Mei 09, 2026 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
TANESCO imesema kuwa lengo la matengenezo hayo ni kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme pamoja na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wateja wake.
Maeneo yatakayokumbwa na ukosefu wa huduma ya umeme ni pamoja na Wilaya ya Njombe, Wilaya ya Makete, Wilaya ya Wanging’ombe pamoja na Wilaya ya Makambako.
Aidha, TANESCO imewaomba wananchi na wateja wake kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha matengenezo huku ikiahidi kuendelea kuboresha huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya wananchi na shughuli za kiuchumi.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Magereza Road, Chaugingi Street
Njombe